Viumbe watano wanaopewa heshima jeshini mbali na binadamu

Kwa kawaida wanyama hurahisisha maisha ya wanadamu kwakuwa walinzi wetu, chakula chetu na usafiri wetu lakini kuna baadhi ya wanyama na ndege walioweza kujiwekea heshima duniani hasa kwenye sekta maalum za kijeshi na wameweza kupata nafasi za juu jeshini. 1: Sir Nils Olav Nils Olav ni ndege aina ya Penguin alipewa cheo mara ya kwanza mwaka 1972 na kuwekwa kwenye timu ya walinzi wa mfalme Harald V Loudon wa Norway kwa sasa Sir Nils Olav ni Brigedia anapewa heshima zote za kijeshi ikiwemo kupigiwa saluti na kukagua jeshi. 2: Treo Ni mbwa aliyetumikia jeshi la Uingereza kuanzia mwaka 2001 mpaka 2015 , Trio ana medali zisizopungua 63, alipewa medali hizo baada ya kufaya kazi kubwa ya kutegua mabomu na kutambua mahali mabomu yalipo fichwa. 3: William of Orange. William ni njiwa aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la Uingereza mwenye namba MI14, mwaka 1944 William alip...