Posts

Showing posts with the label Biashara

TRA KUMCHUNGUZA ASKOFU KAKOBE

Image
Siku chache baada ya kiongozi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Askofu Zachary  Kakobe kusema kuwa ana fedha nyingi kuliko Serikali, Mamlaka ya Mapato nchini TRA imejipanga kuanza kufuatilia ulipaji wake wa kodi. Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema mamlaka yake imeipokea kwa furaha kauli ya Askofu Kakobe na inataka kujiridhisha vyanzo vya utajiri huo. Kichere amesema TRA inafahamu kuwa shughuli za kidini hazitozwi kodi lakini inataka kufahamu kama fedha hizo za Askofu Kakobe zinatokana na sadaka pekee au kuna shughuli nyingine za kiuchumi. "Tumefuatilia hakuna kumbukumbu za Askofu Kakobe kulipa kodi, sasa tumeona tumfuate maofisa wetu wakajiridhishe kama fedha hizo anazozizungumzia zinatokana na sadaka," "Na kama hana shughuli zozote za kiuchumi ikiwa ina maana utajiri huo unatokana na sadaka ni jambo la kushtua kidogo lakini sisi tutaishia hapo," Amesema katika taarifa za mamlaka hiyo wapo watu wengi wenye fedha nyingi na k...

Jinsi ya kuanzisha Biashara bila Mtaji

Image
Wengi huamini kuwa lazima uwe na fedha ndiyo uanzishe biashara na ndiyo sababu yao kuu ya kukaa bila kujishughulisha. Ukweli ni kwamba mtaji ni moja ya kitu muhimu katika kuanzisha biashara, lakini kuna aina ya biashara ambazo zinahitaji gharama ndogo kuanzisha na kukupelekea kupata faida kubwa. Kama mfanyabiashara unaweza kutoka kwa kishindo kwa kuanza ukiwa huna kitu na kufanya kazi kwa juhudi ukiwa upande wa huduma na kufanikiwa kutengeneza faida kubwa na kutokea hapo na kuanza kufikiria kuanza kukodi ofisi yako, kuajiri watu wengine na kadhalika. Ingawa ni rahisi kutoka ukiwa upande wa huduma lakini inahitaji ujuzi au weledi fulani hivi ili uweze kufika kilele cha mafanikio. Hapa simaanishi lazima uwe umesoma chuo kikuu maana ujuzi au utaalamu wa jambo halihusiani na digrii ya chuo kikuu. Unaweza pata ujuzi kwa kuhudhuria semina na warsha mbalimbali au kufundishwa na mtu mwenye ujuzi husika na baada ya kupata ujuzi kuanza kuufanyia kazi katika maisha yako ya kawaid...