Posts

Showing posts with the label habari

MATOKEO YA UCHAGUZI: DKT. MOLEL AIBUKA KIDEDEA UBUNGE SIHA

Image
Mgombea Dkt. Godwin Mollel (CCM) ameibuka mshindi wa kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro uliofanyika jana Jumamosi, Feb 17, 2017. Ikitangaza matokeo hayo, Tume ya Uchaguzi (Nec), imesema Dkt. Mollel amepata kura 25,611 dhidi ya kura 5,905 alizopata Elvis Mosi wa CHADEMA, kura 274 alizopata Tumsifueli Mwanri wa CUF na kura 170 alizopata Azaria wa SAU. Asante kwa kutembelea mashele blog

WATU MAARUFU WALIOGUSWA NA TUKIO LA MWANAFUNZI ALIYEPIGWA RISASI

Image
Taarifa za kifo cha mwanafunzi Aquillina Akwilini aliyepigwa risasi kifuani na Polisi na kupoteza maisha jana February 16, 2018 akiwa kwenye daladala zinaendelea kuenea kwenye mitandao ya kijamii. Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati Askari Polisi wakiwatawanya wafuasi wa upinzani waliokuwa wakifanya maandamano katika eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam. Watu maarufu mbalimbali wameandika kwenye mitandao yao ya kijamii na kuonesha kuguswa na tukio hilo la kuuawa kwa Binti huyo, ikiwa ni pamoja na Mwanamuziki Shilole, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe na Mwandishi wa Habari za Michezo Edo Kumwembe.

Sanduku la Kupigia Kura Laibiwa Kinondoni

Image
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CHADEMA) Salum Mwalimu amedai sanduku la kupigia kura katika mtaa wa Idrisa Magomeni Jijini Dar es Salaam limeibwa huku watu wakishuhudia kitendo hicho kikifanyika na hakuna hatua zozote za kisheria zilizofanyika Salum Mwalimu amebainisha hayo pindi alipokuwa anazungumza mubashara kutoka katika kituo hicho baada ya kupata taarifa kutoka kwa mmoja wa wakala wake aliyempigia simu kumtaarifu kwamba kuna mtu ameiba sanduku la kupigia kura akiwa na gari na kutokomea pasipo julikana. "Nimepigiwa simu na wakala wangu kuwa sanduku lilikuja na kuibwa lakini nikazungumza na msamamizi wa kituo hichi pamoja na Polisi ambae ni msamimizi mkuu wote walikiri kuwa sanduku limeibwa na kwa pamoja wote tulikubaliana kuwa sanduku liliibwa na mtu ambae alikuja na kulipora japo watu walikuwa wamekaa hapa hapa akatokomea nalo", amesema Salum. Pamoja na hayo, Salum Mwalimu ameendelea kwa kusema "baada ya dakika kama 10 hivi sanduku likar...

MABASI 70 YA MWENDOKASI YAMWAGWA DAR

Image
   Moja ya mabasi ya mwendokasi likishushwa kutoka kwenye meli. Shughuli ya kuyashusha mabasi hayo ikiendelea. Muonekano halisi baada ya kushushwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Udart, Charles Selemani akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea mabasi hayo. Meli iliyobeba mabasi ya mwendokasi kama inavyoonekana ikiwa bandarini jijini Dar. KAMPUNI itoayo huduma ya usafirishaji wa abiria kwa mabasi ya mwendo wa haraka jijini Dar,(Udart) imeingiza mabasi mapya 70 na kuyapokea bandarini jijini Dar katika kuhakikisha inaongeza nguvu na kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wateja wake. Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuyapokea mabasi hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Udart, Charles Selemani amewashukuru wakazi wa Dar kwa kuendelea kutumia usafiri huo na kwamba wazidi kuwa na imani juu yao ikiwa ni pamoja na kuwa wavumilivu kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na usafiri huo kwani siku si nyingi mikakati hiyo itakamilika. Aidha, B...

Huyu ndiye Rais mpya wa Afrika kusini

Image
BUNGE la Afrika Kusini limemchagua Mwenyekiti wa chama tawala cha ANC Cyril   Ramaphosa, kuwa Rais wa mpito wa nchi hiyo, mpaka pale uchaguzi utakapofanyika baada ya rais wa taifa hilo Jacob Zuma kujiuzulu. Zuma alikuwa akikabiliwa na tuhuma nyingi, moja ikiwa ni kumhusisha na vitendo vya rushwa japokuwa mwenyewe amekanusha kuhusishwa na tuhuma hizo.  Alijiuzulu mara moja jana jioni licha ya kusema hakubaliani na uamuzi wa chama                             Tangazo.    

KARANI WA BODI YA MITIHANI ADAI NYOKA AMEKULA MILIONI 227 ALIZOKUSANYA

Image
Karani mmoja wa Bodi ya Mitihani nchini Nigeria, Philomena Chieshe amefukuzwa kazi baada ya kuwaambia wakaguzi wa hesabu kuwa nyoka alikula naira milioni 36 ambazo ni dola 100,000 (Tsh milioni 227) alizokuwa amekusanya. Bodi hiyo ya mtihania imesema kuwa imeyakataa madai yake na imeanisha kumchukulia hatua za kinidhamu. Kisa hicho kimezua shutuma na dhihaka kwenye mitandao ya kijamio nchini Nigeria. Nayo tume ya kupambana na rushwa nchini Nigeria iliandika ujumbe huu katika Twitter ambayo nembo yake ni mwewe.

Binti wa Kifaransa aliyekulia msituni na Wanyama

Image
Sio filamu wala maigizo, hii ni kweli tupu, fahamu historia ya binti wa Kifaransa aliyekulia msituni na wanyama na kucheza nao kama anavyocheza na binadamu bila kumdhuru, mpaka akaanza ku-adopt tabia zao. Anafahamika kwa jina la Tippi Benjamine Okanti Degré alizaliwa tarehe 4 Juni 1990, huko Windhoek Namibia, akiwa ni mtoto wa pekee wa mpiga picha za wanyama na mtengeneza filamu wa Kifaransa, Sylvie Robert na Alain Degre. Katika utoto wake Tippi alikulia katika nchi ya Namibia kwenye mbuga za wanyama na watu wa kabila la Bushman, ambako wazazi wake walikuwa wakifanya kazi ya kupiga picha na kutengeneza documentary za maisha ya wanyama, kitendo ambacho kilimfanya kuwa karibu na wanyama kwa kuwa hakuwa na watu wa kucheza ano. Maisha ya Tippi yalikuwa ya kuzungukwa na wanyama wanaojulikana kwa ukali na kutokuwa na urafiki na binadamu, wakiwemo simba, chui, mamba, nyoka, tembo, na kila mnyama mabaye unajua anapatikana kwenye mbuga za Afrika. Kwenye miaka 10 ya utoto wake Ti...

Vijiji 100 kupata maji ya Ziwa Victoria

Image
WIZARA ya Maji na Umwagiliaji inatekeleza mradi wa maji wa vijiji 100 vilivyopo kandokando ya bomba kuu kutoka Ziwa Victoria hadi Kahama Shinyanga, Bunge limeelezwa. Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Jumaa Aweso, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Msalala (CCM), Ezekiel Maige. Katika swali lake, Maige alitaka kujua ni vijiji vingapi kati ya hivyo 100 hadi sasa vimepatiwa maji. “Je, Serikali itafikisha lini Maji ya Ziwa Victoria katika vijiji vya Mwakazuka, Mwaningi, Kabondo, Ntundu, Busangi, Buchambaga, Nyamigege, Gula, Izuga, Buluma, Matinje na Bubungu,” alihoji Mbunge huyo. Akijibu swali hilo, Aweso alisema utekelezaji huo unafanywa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.Alibainisha katika awamu ya kwanza jumla ya vijiji 40 vilivyopo katika Halmashauri za Msalala, Misungwi, Kwimba na Shinyanga vimetambuliwa na ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji 33 umekamilika na baadhi ya vijiji vingine vinaendelea na ujenzi. Aidha, Aweso alisema vij...

WATOTO 6 WAJITOKEZA KUGOMBEA UGAVANA , MAREKAN

Image
Jimbo la Kansan nchini Marekani hivi karibuni limepitisha sheria ya kutoangalia kigezo cha umri kwa atakayejitokeza kugombea nafasi ya ugavana kwenye jimbo hilo jambo lililotengeneza mwanya kwa watoto pia kutangaza kugombea. Mpaka sasa watoto wa kiume 6 walio chini ya umri wa miaka 18 wamejitokeza kuchukua na kujaza fomu za kugombea Ugavana kwenye jimbo hilo mwezi November mwaka huu. Watoto hao ni pamoja na Tyler Ruzich wa chama cha Republican, Aaron Colman wa Independent, Joseph Tutera Jr., wa Republican, Dominic Scavuzzo, pia wa Republican, Ethan Randleas wa Libertarian na Jack Bergeson wa Democrat.

Tigo wapunguza gharama

Image
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo imepunguza gharama za kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kitaifa na kimataifa kwa asilimia 27.5. Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kuwapo kwa punguzo hilo katika robo ya nne ya mwaka iliyoishia Desemba 2017 ikilinganishwa na robo ya tatu ya mwaka ulioishia Septemba. Ripoti ya robo ya tatu ilionyesha kuwa Tigo ndiyo mtandao wenye gharama kubwa Tanzania katika kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi kitaifa na kimataifa jambo ambalo limekuwa tofauti na robo ya nne ya mwaka. Katika robo ya tatu ya mwaka wateja wa Tigo walikuwa wakilipia Sh360 kwa dakika (kabla ya VAT) katika kupiga simu ndani ya mtandao ambayo imeshuka hadi kufikia Sh261 katika robo ya nne ya mwaka, ikiwa ni pungufu ya Sh99 sawa na asilimia 27.5. Hata hivyo, kushuka kwa gharama za kupiga simu ndani ya mtandao katika robo ya nne, takwimu zinaonyesha kuwa  tozo za Tigo bado zipo juu ya wastani wa gharama za kupiga simu a...

Odinga ataka uchaguzi mwingine tena

Image
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya kupitia NASA, Raila Amollo Odinga, ametaka kufanyika kwa uchaguzi mkuu mpya tena mwezi Agosti mwaka huu 2018. Akizungumza na BBC Raila Odinga amesema hamtambui Uhuru Kenyatta kama Rais wa nchi hiyo kwani hana kibali cha watu, ingawa hana lengo lolote la kupambana na serikali ya Kenyatta. "Hatutamtoa Uhuru Kenyatta Ikulu anaweza kuendelea kukaa kwa amani, lakini hatuutambui Urais wake kwa sababu uko kinyume, tunataka uchaguzi mwingine na kwa mujibu wa ratiba yetu utakuwa Agosti mwaka huu”, amesema Raila Odinga. Hivi karibuni kiongozi huyo wa upinzani nchini Kenya alijiapisha na kuwa Rais wa watu, akisema yeye ndio chaguo la watu kuwaongoza na sio Uhuru Kenyatta.

Moto wateketeza bweni la wanafunzi

Image
Mwanza.  Jengo la bweni la wanafunzi wa kiume katika shule ya Sekondari Katunguru wilayani Sengerema mkoani Mwanza limeteketea kwa moto. Kuteketea kwa jengo hilo lililogawanywa katika sehemu tatu kumewakosesha malazi wanafunzi zaidi ya 200 wa shule hiyo. Mkuu wa shule hiyo, Baraka Msimba amesema moto huo ulianza saa tatu usiku wa kuamkia leo. “Hadi sasa hasara iliyosababishwa na moto huo inakadiriwa kuwa zaidi ya Sh70 milioni,” amesema Msimba na kuongeza: “Hakuna mali ambayo imeokolewa ikiwemo madaftari, vitabu, magodoro, blanketi, mashuka na nguo za wanafunzi. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema, Magesa Mafuru amesema ofisi yake inafanya kila linalowezekana kuwasaidia wanafunzi hao ili waendelee na masomo. “Wakati halmashauri ikiendelea na juhudi za kurejesha hali ya kawaida shuleni hapo, naiomba jamii kila mmoja mwenye uwezo kujitokeza kuwasaidia wanafunzi hawa kuendelea na masomo na maisha ya kawaida,” amesema Mafuru. Mwananchi:

Mose Iyobo awachezeshea kichapo Shilawadu

Image
 Watangazaji wa Kipindi maarufu cha Shilawadu kinachorushwa na Clouds tv,Soudy Brown na Kwisa wamechezea kichapo kutoka kwa Dancer wa Diamond,Mose Iyobo,usiku wa kuamkia  ijumaa,baada ya kutaka kumuhoji kuhusu matukio yaliyotokea hivi karibuni kati ya familia yake na mwanadada Tunda. Wakithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Shilawadu wameandika katika ukurasa wao wa instagram: Kazi yetu ina changamoto kubwa sana..asilimia kubwa ya ma star wanatuunga mkono. Usiku wa Leo wakati tukiwa kazini tumenusurika kumwagwa damu na mtu tuliemfuata kumuomba kufanya naye mahojiano,kati yetu kuna walioumia viuno,mikono, etc.kuna uharibifu wa vifaa vyetu vya kazi umetokea pia,wenzetu wanaendelea na matibabu Mungu  ni mwema  Mungu ni wetu sote na hili litapita bado tuna wasiwasi tu kama mhusika ataendelea kututafuta kwa ajili ya kutudhuru zaidi,tunasikitishwa sana na matumizi ya nguvu dhidi yetu sisi Wanyonge #Shilawadu Kuna watu watasema Shilawadu wamezidina kusahau kuwa...

Breaking News: Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia

Image
Habari tulizozipokea hivi punde zinasema kuwa mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 2,2018 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam. Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita. Mke wa Kingunge Peras Ngombalemwiru alifariki dunia mwanzoni mwa mwezi January kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo.  Mzee Kingunge alikuwa kiongozi mwandamizi nchini Tanzania katika serikali za awamu nne zilizopita na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali  zikiwemo ukuu wa mikoa ya Tanga na Singida, Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi na Waziri katika wizara mbalimbali

UNHCR Yadai wakimbizi 1,200 wakimbilia Tz kutoka Congo

Image
  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi la UNHCR, limedai kuwa jumla ya wakimbizi 1200,raia wa jamhuri ya Demokrasia ya Congo,wameyakimbia mapigano yanayoendelea Mashariki mwa nchi hiyo na kuingia Tanzania. Aidha shirika hilo limedai Maelfu ya watoto, wanawake na wanaume, wameacha makazi yao kukimbia mapigano dhidi ya makundi yenye silaha ya Mai Mai yanayoendelea Kusini mwa Jimbo la Kivu. Aidha shirika hilo la umoja wa mataifa limedai mbali na Tanzania,wakimbizi wengine wamekimbilia nchi za Burundi, na Uganda. Wakati huo huo, inaamika kwamba, kuna wimbi kubwa zaidi la wakimbizi ambao wapo Kivu Kusini wakiwa katika hali mbaya ya kukosa chakula na makazi.

Umri wa Kustaafu Kwa Madaktari Bingwa, Wahadhiri Waandamizi na Maprofesa Sasa miaka 65.

Image
Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswaada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298  (The Public Service Act) itakayowezesha muda wa kustaafu kwa  Wahadhiri waandamizi, Maprofesa na Madaktari Bingwa kuwa miaka 60 kwa hiari na lazima miaka 65. Akizungumza wakati akiwasilisha muswaada huo  Mwanasheria  Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju amesema kuwa marekebisho katika jedwali yanapendekeza kuongezwa kwa kifungu kipya cha 25A ambacho kinaainisha kuhusu umri wa kustaafu ambapo kwa sasa sheria ilivyo  haina masharti hayo isipokuwa umri wa kustaafu umetajwa katika sheria zinazoanzisha mifuko ya hifadhi za jamii. Aliongeza kuwa, uzoefu umeonyesha kuwamba Maprofesa na Wahadhiri waandamizi wa vyuo  Vikuu  vya Umma pamoja na madaktari Bingwa wa Binadamu wa Hospitali za Umma wamekuwa wakihitajika kuendelea kutoa huduma, utaalamu na ...

Serikali imezima matangazo ya Television Kenya

Image
  Wakati wafuasi wa Muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA) wanaendelea na shughuli ya kuapishwa kwa Raila Odinga kuwa ‘Rais’ serikali nchini humo imepiga marufuku TV za Kenya kurusha LIVE matangazo hayo kutoka katika uwanja wa Uhuru Park TV hizo ni Citizen, KTN na NTV. Wafuasi wa Upinzani tayari wamekwisha fika katika uwanja wa Uhuru Park kushuhudia tukio hilo Inaelezwa kuwa serikali nchini Kenya ilikuwa imekwisha tahadharisha kuhusu vyombo vya habari nchini humo kurusha live matangazo hayo ya Odinga kuapishwa ambapo ni kinyumme cha sheria. Hata hivyo vyombo vya habari vya kimataifa havijafungiwa na vinaendelea kurusha matangazo hayo kama kawaida.

BREAKING: Raila Odinga Ajiapisha Kuwa ‘Rais wa Wananchi wa Kenya’

Image
Kiongozi  wa upinzani Raila Odinga (NASA) ameapishwa kuwa ‘Rais wa Wananchi’ wa Kenya licha ya kugomea uchaguzi mkuu wa marudio nchini humo. Raila Odinga amefika  leo katika Uwanja wa Uhuru Park pamoja na viongozi wengine wakuu wa NASA akiwemo Moses Wetangula na Musalia Mudavadi na kujiapisha akishika Biblia. Aidha, mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa Chama Cha Wiper hakuwepo wakati wa kuapishwa kutokana na kuhofia kukamatwa, ambapo Odinga amesema ataapishwa baadaye. “Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya, hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya, maelekezo mengine mtayapata baadae,” alisema Odinga baada ya kuapishwa. Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ‘ si mapinduzi ya serikali’ Raila aligomea uchaguzi huo kwa sababu za kusema kuwa tume ya Uchaguzi nchini humo si ya Uhuru na haki. Uchaguzi huo wa marudio ulikuja baada ya Mahakama ikiongozwa na Jaji Maraga kutengua Uchaguz...

WAZIRI JAFO, MADARASA YA TEMBE, UDONGO, NYASI, YASITUMIKE KATIKA SHULE YEYOTE NCHINI

Image
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwenye maeneo yao bado kuna wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama yalioezekwa Nyasi au kujengwa kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja kutumia madarsa hayo na kujenga madarasa bora. Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kujenga uwezo wa viongozi kuweza kutawala kwa ufanisi. “Viongozi wangu nataka Mkakusanye mapato ya ndani kwa nguvu zote na Fedha hizo mzitumie kwenye miradi ya maendeleo na kwa wale ambao mpaka leo wanafunzi wanasomea kwenye mazingira duni hawana madarasa bora watoto wanasomea kwenye madarsa ya Tembe, mengine yameezekwa kwa Nyasi nahitaji muelekeze Nguvu katika ujenzi wa madarasa bora na hayo ya Tembe yotoweke kabisa; M...

Umeme kukosekana Mbagala, Kurasini, Bandari

Image
  Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema njia ya kusafirisha nishati hiyo ya Ilala -Kurasini itazimwa kwa muda kupisha matengenezo ya dharura. Taarifa ya Tanesco iliyotolewa leo Jumamosi Januari 27,2018 kwa wateja wa Mbagala, Kurasini na Bandari imesema njia hiyo itazimwa kwa muda wa saa tatu kuanzia saa nne asubuhi. Maeneo yatakayo athirika yametajwa kuwa ni yote ya Mbagala, Kurasini na Bandari. Tanesco imewatahadharisha wananchi kutoshika waya uliokatika.