Posts

Showing posts with the label Mwansoko

MWANSOKO 1991 MTINDO WA KITAALUMA

Image
Sura ya 2: Mtindo wa kitaaluma Utangulizi Uzoefu wa kusoma makala za kitaaluma na kuhudhuria semina mbalimbali umeonyesha kuwa pamoja na maudhui mazuri ya makala hizi kumekuwa na ukiukaji wa kutosha wa taratibu za kimtindo ambazo zina nafasi muhimu sana katika maandiko na majadiliano yoyote ya kitaaluma. Ingawa mwandishi amekuwa akitoa madokezo ya hapa na pale katika semina hizi kuhusu kanuni za kimtindo na makosa yatokanayo na ukiukaji wa taratibu hizi, hata hivyo suala hili bado linahitaji kuchukuliwa kwa uzito wake kamili hasa kutokana na kuongezeka kwa dhima ya Kiswahili baada ya lugha hii kufanywa lugha ya taifa. Matokeo ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya taifa yamekuwa ni uimarishwaji zaidi wa lugha hii ikiwa ni pamoja na kuipenyeza katika matumizi ya kitaaluma. Masuala ya kitaaluma kwa kawaida hayawi ya nchi moja tu peke yake, bali huhusisha na kushirikisha mataifa mbalimbali. Hii ina maana kwamba tuandikapo makala au vitabu vyetu vya taaluma mbalimbali katika Ki...

TOFAUTI ZA KIMTINDO KATI YA MZUNGUMZAJI MMOJA NA MWINGINE

 Je nikweli kuwa kuna utofauti katika mazungumzo baina ya mzungumzaji mmoja na mwingine?.... info.masshele@gmail.com Jibu  ni ndio , na tofauti hizo katika uzungumzaji huweza kuchangizwaa na mambo kadhaa Mwansoko 1991 anasema " Na hii ina maana kwamba kunahaja ya kuziangalia zile sababu zinazoathiri maumbo ya maneno katika mawasiliano na uchaguzi wa zana za kiisimu zitakazotumiwa na mwandishi au mzungumzaji. Sababu hizi hugawanyika katika mafungu mawili makubwa.: 1. sababu dhahania  (subjective factors) 2. sababu yakini  (objective factors) Baadhi ya sababu dhahania ni: 1. hali za kiuchumi na kijamii za washiriki wa mawasiliano (kazi zao, elimu yao, tabaka lao katika jamii... n.k.) 2. hali ya kisaikolojia ya wawasilianao (k.m. tabia zao) 3. jinsi mtu anavyojisikia  (mood) wakati wa mawasiliano (mwenye furaha? huzuni? majonzi? wasiwasi?) 4. rika (umri) la washiriki katika mawasiliano. Ni kweli kabisa kwamba namna ya uzungumzaji wa mt...

Mwansoko 1991 Mitindo ya kiswahili sanifu pdf

Image
H.J.M. Mwansoko DAR ES SALAAM UNIVERSITY PRESS DAR ES SALAAM Dar es Salaam University Press S.L.P. 35182 Dar es Salaam ©  H.J.M. Mwansoko Chapa ya Kwanza, 1991 ISBN 9976 60 161 1 Haki zote zinaehifadhiwa. Hairuhusiwi kuigiza, kunakili au kukitoa kwa njia yoyote ile bila idhini kwa maandishi ya Dar es Salaam University Press. Sura ya 1: Elunumitindo na mitindo @masshele Elimumitindo Kabla hatujaeleza fasiri au maana ya elimumitindo ni muhimu kuanza kueleza taaluma hii inashughulikia nini. Jaribio dogo lifuatalo huenda litasaidia: Tuseme kwa mfano inatolewa tathmini ya maendeleo ya kazi ya mchunguzi (mtafiti) mmojawapo wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili katika mazingira mawili tofauti. Katika mazingira ya kwanza (1) tathmini htyo inatolewa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo mbele ya Kamati ya Tathmini za wanataaluma na katika mazingira ya pili (2) tathmini hiyohiyo inatolewa na marafiki wawili wa mchunguzi huyo katika mazungumzo yao yasiyo rasmi, yaani maongezi ya k...

MWANSOKO 1991 MTINDO WA MAWASILIANO YASIYO RASMI

Image
@mashele Sura ya 5: Mtindo wa mawasiliano yasiyo rasmi Utangulizi Hadi sasa mitindo tuliyoijadili ni ile ambamo mawasiliano yanatekelezwa katika mazingira yaliyo rasmi, yaani yanayowalazimisha wanaowasiliana kufuata taratibu au kanuni maalum za matumizi ya zana za kiisimu. Lakini katika hali ya kawaida ya maisha si muda wote binadamu anakuwa kwenye mazingira yanayomtaka awasiliane kirasmi. Na kwa kweli idadi kubwa ya mawasiliano yanayofanywa na wanadamu hufanywa kwenye mazingira yasiyo rasmi. Sura hii itayaainisha mazingira hayo pamoja na zana za kiisimu zinazotumika katika mawasiliano yasiyo rasmi. Mawasiliano Yasiyo Rasmi Mawasiliano yasiyo rasmi ni yale maongezi ya kawaida ya kila siku mathalani nyumbani (yaani mazungumzo kati ya baba, mama, watoto, watumishi wa nyumbani n.k.), baina ya wasafiri kwenye vyombo vya umma vya usafiri, kama vHe mabasi, magarimoshi, meli n.k., baina ya marafiki mitaani, michezoni, kwenye tafrija au kumbi mbalimbali za starehe, kama v...