Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 01 na 02

Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA Ilisikika sauti ya mwanamke akilia kwa sauti kali sana ndani ya sekunde chache.....kisha sauti hiyo ikatulia kimya....baada ya sekunde kumi ikasikika sauti ya mtoto mchanga akilia.....baada ya dakika kumi kupita,,zikasikika sauti zikisikika zikisema"sukuma kwa nguvu....usibane mapaja utamuuwa mtoto...ghafla ikasikika sauti ikisema ""mama weee... baada ya sekunde tatu hivi ikasikika sauti tena ya mtotochanga akilia....mwanamke huyo aitwae Rose alijifungua watoto mapacha wote wa kiume.walipishana dakika kumi za kuzaliwa...Rose alifurahi sana..Akamshukuru Mungu kwa kujifungua salama...baada ya masaa mawili kupita alikuja mumewe aitwae SEBA....alifurahi sana akasema,nitakupa zawadi mke wangu..nakuahidi nitakununulia gari...Rose alifurahi sana kusikia kauli hiyo ya mumewe.. *************** kesho yake majira ya saa nne za asubuhi.. madaktari walimruhusu Rose kwenda nyumbani..kutokana Rose alikuwa na nyonga pana sana hivy...