Posts

Showing posts with the label nyakiru

Nyakiiru Kibi pdf-2

Image
Fasilu ya Tatu Taswira 615 Habari ilienea Watu wakaisikia Kawamara wametua Vijana wa kuvutia. 616 Wana mioyo ya wema Wanagawa bure nyama Na adabu na heshima Na nguo wamevalia. 617 Kwa kasi ilisambaa Habari ikazagaa Watu wakaja manria Wageni kuangalia. 618 Habari ikasaflri Hadi katika kasiri Ya Omukama amiri Ntumwa akaisikia. 619 Akataka sulutani Waitwe mara wageni Kuwahoji atamani Ajue walichojia. 620 Akapelekwa tarishi Mwenye mbio mtumishi Aupeleke utashi Wa mkuu wa jamia. 621 Mithili ya mbayuwayu Akenda mjumbe huyu Anahema kama   kuyu Kwa mbio kuzidmua. 622 Kwake Nyakiru mgeni Kabisha kangia ndani Akisha  subalherini Amri kaitongoa. 623 “Mtukufu Omukama Simba anayenguruma Mume wa waume wema Wageni awamkia. 624 “Mtukufu wajamala Anasema  halahala Leo msende kulala Kabula ya kumwendea. 625 “Mtukufu utashiwe Leo mfike mpewe Atakayo muambiwe Na kisha mtarejea.” 626 Akaridhi muungwana “Twashukuru ...