FUMANIZI

*FUMANIZI* (Sehemu ya III) *©Mwafrika Merinyo* Fatima hakuelewa chanzo cha maradhi haya yaliyomsibu Himid na hakutaka hata kujua. Alishamuuliza mumewe kama amewaona matabibu na jibu la mumewe likawa kwamba wataalam wamemweleza kuwa hana tatizo, ni hali ya kupita tu. Na sasa Fatima hakujali kuhusu hali ya Himid, kwani alikwishaona kuwa hapa ndoa haiwezi kuwepo. Alishawasiliana na bi mkubwa Salama, mke wa kwanza wa Himid, kuulizia kuhusu shida hii ya mume wao. Naye Salama akakiri kuwa kuna tatizo, ila kwa mawazo ya bi Salama Himid haelekei kujishughulisha na tiba yoyote. Mwaka wa pili baada ya mchezo wa vidole kuanza, Fatima alichoka, akihisi kuwa anajitesa bila sababu. Kuomba talaka akahofia kuwa angeonekana mkorofi, kwa kuwa wenzake wawili walikuwa wanaendelea kuvumilia. Lakini kwa umri wake wa miaka arobaini na uzao wa mtoto mmoja tu, akajihisi mhitaji sana na asiye na msaada. Katika hali ile, na katika kuwa na maelewano ya kirafiki kati yake na Rama, mmoja wa wateja wake wa bia...