Jinsi ya kukabiliana na mambo yanayozuia wasichana kuwa wabunifu Tanzania
Ni pamoja na kuondia vikwazo vya kitamaduni na wasichana waanze waamke na kujitoa. Wadau watakiwa kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa sahihi kwa wasichana. Pia wametakiwa kutatua changamoto za jamii yao. Kilimanjaro. Licha ya juhudi mbalimbali za Serikali na wadau wa maendeleo kuwawezesha wasichana wengi kuingia katika fani ya sayansi, bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazowakwamisha kuwa wabunifu. Changamoto hizo zikiwemo za mifumo na utamaduni zinawazuia wasichana kuonyesha uwezo na kutoa suluhu za teknolojia zitakazosaidia kuboresha maisha ya jamii. Mei 21 mwaka huu wadau wa ubunifu walikusanyika mkoani Kilimanjaro ili kujadili changamoto zinazokwamisha ubunifu miongoni mwa wasichana na namna ya kuwasaidia kujikwamua na wakatumia ubunifu huo kutoa suluhu zitakazosaidia kuboresha maisha ya jamii. Mwanzilishi mwenza wa jamii ya wadau wa ubunifu ya Startup Grind Kilimanjaro, Dorcas Mgogwe amesema ubunifu miongoni mwa wasichana upo chini kut...