TAMTHILIYA LINA UBANI &UHAKIKI

Miongozo ya Lugha na Fasihi MIONGOZO ya Lugha na Fasihi ni mfululizo uliokusudiwa wanafunzi na watpenzi wa lugha na fasihi ya Kiswahili. Mfululizo huu umebuniwa kutokana na lengo la kuwasaidia wanafunzi wa hjjha na fasihi katika ngazi mbalimbali za taaluma zao, hasa wale wanaojiandaa kwa mitihani ya Taifa. Mfululizo huu utatoa vijitabu ambaVyo vitakuwa vinasaidia kuchambua vitabu vya lugha na fasihi ambavyo vimeteuliwa na Wizara ya Elimu vitumike kuwatahini wanafunzi katika vyuo na sekondari nchini. Kwa hali hiyo, mfululizo huu utajumuisha uchambuzi wa vitabu vilivyochapishwa na Dar es Salaam Umvereity Press (DUP) na vile ambavyo vitakuwa vimechapishwa na mashirika raengine. Uchambuzi wa kila kitabu utazingatia fani na maudhui yanayojitokeza katika kazi hiyo, na mwishoni kuna maswali ambayo yanamwongoza mwanafunzi. Miongozo hii imeandaliwa kwa kuzingatia utaalamu wa hali ya juu ili kurahisisha usomaji wa kitabu kinachohusika. Wanafunzi na wapenzi wa lugha na fasihi...