Fasihi ya kiswahili ni zile kazi za kiufundi na kisanaa zilizo andikwa au kusemwa  zitumiazo lugha ya kiswahili, utamaduni wa mswahili au pengine mtunzi kuwa mswahili, na zinazowahusu waswahili, kwa lengo la kufikisha ujumbe fulani.

Tunazo kazi kadhaa za kifasihi kama vilie 
-Nyimbo
-Ushairi
-Riwaya
-Tamthiliya
-Hadithi
-Utenzi
-Tendi
-Methali
-Vitendawili
-Nyambi
-Matangazo ya biashara( kwa mujibu wangu)
N.k.

Je mwanamke anatazamwa vipi katika fasihi ya kiswahili?

Wanawake wamekuwa wakifasiliwa kwa namna tofauti tofauti katika kazi za kifasihi, hasa kulingana na mtunzi Wa kazi hiyo na Jamii anayotoka.
Mathalani, ukichunguza kazi za E. Mbogo hasa zile za Malkia Bibi titi Mohammed, Morani na Watoto wa mama ntilie utagundua kuwa Emanuel mbogo anamtazama mwanamke tofauti na watunzi wengine wanavyomtazama kama vile, P.Muhando katika kazi za Nguzo mama, Pambo, na ile ya Tambueni haki zenu.

Kazi za kifasihi zinazomsawiri mwanamke kichanya wanampa uhusika ufuatao,
-Kiongozi bora
-Jasiri, mpambanaji, mzalendo, mlezi, mwenye kutoa ushauri,  anayefanya kazi kwa bidii nk

Wakati zile zinazo msawiri mwanamke kihasi 
-Chombo cha starehe
- Mtegemezi
-Hawezi
-Hana elimu
-Kazi za nyumbani n.kk
mwisho unaweza kuendeleza mjadala huu kwa kutaja jina, skuli utokayo, na mchango wako katika sehemu ya comment.
www.masshele.blogspot.com