KUFANYA MAZOEZI KIPINDI CHA UJAUZITO JE NI SALAMA?

1. UMUHIMU WA MAZOEZI KIPINDI CHA UJAUZITO 2. MAZOEZI YA MAMA MJAMZITO 3. JINSI YA KUFANYA MAZOEZI UKIWA NA MIMBA Kufanyaa mazoezi ni jambo ambalo binadamu wengi hulifanya mara kwa mara ikiwa ni mpango wa kimaisha au hulifanya mara moja moja. Mazoezi ni kitendo cha kuushughulisha mwili kwa njia mbalimbali. Mazoezi yaliyojipatia umaarufu ni kama kutembea, kukimbia, kushiriki michezo mbalimbali na hata watu hutumia vifaa maalumu vya mazoezi kuishughulisha miili yao. Hivi karibuni vituo vingi tuu vya mazoezi ambavyo vilikuwa maarufu kwenye nchi zilizoendelea vinaanza pia kuonekana barani Afrika. Mazoezi ni mazuri kwa afya ya mwili na akili. Na pia mazoezi yanahusishwa kabisa kisayansi kwenye jedwali la kupata afya bora. Ikiwa ni kawaida kabisa watu wa umri wowote ule kushiriki katika mazoezi, huwa inazua mjadala mara kwa mara ni kwa namna gani wajawazito wafanye mazoezi. Kwanza kabisa je wanaruhusiwa kisayansi kufanya mazoezi? Waandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya DW waliwahi kuya...