Posts

Showing posts with the label Siasa

MATOKEO YA UCHAGUZI: DKT. MOLEL AIBUKA KIDEDEA UBUNGE SIHA

Image
Mgombea Dkt. Godwin Mollel (CCM) ameibuka mshindi wa kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro uliofanyika jana Jumamosi, Feb 17, 2017. Ikitangaza matokeo hayo, Tume ya Uchaguzi (Nec), imesema Dkt. Mollel amepata kura 25,611 dhidi ya kura 5,905 alizopata Elvis Mosi wa CHADEMA, kura 274 alizopata Tumsifueli Mwanri wa CUF na kura 170 alizopata Azaria wa SAU. Asante kwa kutembelea mashele blog

Sanduku la Kupigia Kura Laibiwa Kinondoni

Image
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CHADEMA) Salum Mwalimu amedai sanduku la kupigia kura katika mtaa wa Idrisa Magomeni Jijini Dar es Salaam limeibwa huku watu wakishuhudia kitendo hicho kikifanyika na hakuna hatua zozote za kisheria zilizofanyika Salum Mwalimu amebainisha hayo pindi alipokuwa anazungumza mubashara kutoka katika kituo hicho baada ya kupata taarifa kutoka kwa mmoja wa wakala wake aliyempigia simu kumtaarifu kwamba kuna mtu ameiba sanduku la kupigia kura akiwa na gari na kutokomea pasipo julikana. "Nimepigiwa simu na wakala wangu kuwa sanduku lilikuja na kuibwa lakini nikazungumza na msamamizi wa kituo hichi pamoja na Polisi ambae ni msamimizi mkuu wote walikiri kuwa sanduku limeibwa na kwa pamoja wote tulikubaliana kuwa sanduku liliibwa na mtu ambae alikuja na kulipora japo watu walikuwa wamekaa hapa hapa akatokomea nalo", amesema Salum. Pamoja na hayo, Salum Mwalimu ameendelea kwa kusema "baada ya dakika kama 10 hivi sanduku likar...

MBOWE ASIKITISHWA NA KESI YA SUGU INAVYO ENDESHWA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe amedai amesikitishwa na namna inavyoendeshwa kesi ya Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu CHADEMA kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga iliyoahirishwa leo. Freeman Mbowe ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari hii leo katika viunga vya Mahakama ya mkoani Mbeya mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo na kuzitaka mamlaka husika zinazosimamia sheria nchini kujiangalia vizuri katika utendaji kazi wake. "Tumesikitishwa kwa namba suala hili jinsi lilivyo shughulikiwa, sipendi kuingilia uhuru wa Mahakama, mienendo ya kimahakama lakini mimi kama raia na kiongozi nafikili vyombo vinavyostahili kutoa haki kwa wananchi vinawajibu wa kujiangalia vizuri.  "Mahakimu, Majaji, Mawakili wa Serikali pamoja na Askari wenyewe hawa wote ni binadamu haina maana kwamba wao hawawezi kufanya makosa wao ni binadamu kama walivyo wengine", alisema Mbowe. Kesi ...

Wasomi 350 UDSM Wahamia UVCCM

Image
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amepokea jumla ya Wanachma wapya 350 katika Kongamano Maalum lililoandaliwa na Tawi la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Kheri amewataka Vijana wanaopata nafasi za uongozi kuitumia nafasi hiyo kwa ajili ya kuwakomboa wengine na kuacha kutumika na makundi ya watu. “Vijana wengi ambao wameaminiwa wameacha kushughulika na matatizo ya Vijana na yenye tija kwa taifa, wamekuwa wakiendeshwa na watu ambao wanamaslahi yao binafsi” amesema Kheri Amesema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeweza kuwaamini Vijana, hivyo kila kijana wa CCM anabudi kuwaunga mkono viongozi wote Vijana ambao wana nia ya dhati ya kutaka kulifikisha taifa hili pale linapotakiwa liwe. Alimaliza kwa kutoa wito kwa Vijana wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Chaguzi ndogo zinazoendelea na kuifanya CCM ishinde kwa kishindo. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Chama Cha Mapinduzi(UVCCM),Kheri James akizungumza na Wan...

UDSM WAMPONGEZA MAGUFULI

Image
Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) ni serikali ya wanafunzi inayoamini katika sheria, kanuni na taratibu. Lakini pia, ni serikali inayoamini katika kushauri, kuhamasisha na kupongeza kila jambo jema linapotendwa na mtu au kikundi cha watu kwa manufaa ya taifa letu.  Kwa kutumia misingi hii, DARUSO inatumia wasaa huu kutoa pongezi za dhati kwa Mhe. Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuonesha kwake kusikitishwa na baadhi ya watanzania wasiokuwa na nia njema na taifa letu kwa kufikiria kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanzisha mjadala wa kuongeza muda wa Rais kukaa madarakani kitu ambacho hakijawahi kuzungumziwa kwenye kikao chochote halali cha Serikali ya Jamhuri kama hitaji la muhimu kwa taifa letu.  Katika hili, ni wazi kwamba Rais wetu ameonesha mfano wa kuigwa si tu kwa Tanzania bali Afrika na duniani kwa ujumla katika kuheshimu katiba yetu kwa kuwataka wanaoendelez...

TUNDU LISSU KUPELEKWA ULAYA KWA MATIBABU JANUARY 6

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe ameeleza kuwa hali ya Mbunge Tundu Lissu anayepatiwa matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, imeimarika na hivi karibuni atahamishiwa katika hospitali nyingine kwa ajili ya mazoezi ya viungo. “Tiba zote ameshamaliza kinachoendelea sasa ni mazoezi,” amesema Freeman Mbowe. Mbowe amesema hayo leo, Disemba 31, 2017 wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa tarehe 6 Januari, 208 Tundu Lissu atasafirishwa kupelekwa katika nchi moja ya Ulaya ambayo hakuitaja kwa kile kilichotajwa kuwa ni kwa sababu za kiusalama. “Kwa sasa siwezi kuitaja nchi anakokwenda kwa ajili ya usalama,” amesema Mbowe. Amesema gharama zilizotumika hadi sasa kumuuguza ni dola 300,000 za Marekani sawa na zaidi ya Sh 600 milioni. Ikiwa ni siku zaidi ya 100, tokea Mbunge Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi eneo la nyumbani kwake, Area D, Dododma, majira ya saa 7 mchana, akiwa anatokea kazini, kwa sasa hali yake imeimarika ambapo ...

HABARI MPYA: RAIS KUSHITAKIWA MAHAKAMANI

Image
Mahakama ya Katiba nchini Afrika Kusini imebaini kwamba bunge la nchi hiyo lilishindwa kutimiza wajibu wake kwa kushindwa kumuwajibisha rais wa nchi hiyo Ndg. Jacob Zuma juu ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya matumizi mabaya ya fedha za umma. Uamuzi huo wa Mahakama ya Katiba ukiongozwa na Jaji Chris Jafta nchini humo umeainisha kwamba bunge hilo ni lazima lianze mchakato wa taratibu za kumfungulia mashitaka ingawa haikuwa wazi kwamba mchakato huo utaweza kumuondoa madarakani kwa kupigiwa kura. Mahakama hiyo ilikuwa ikisikiliza kesi  iliyofunguliwa na kambi ya upinzani ambayo ilitaka bunge la nchi hiyo kuanza mchakato wa kumshitaki Rais Zuma. Rais Zuma anatuhumiwa kutumia fedha za umma kuendeleza makazi yake binafsi.

TRA KUMCHUNGUZA ASKOFU KAKOBE

Image
Siku chache baada ya kiongozi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Askofu Zachary  Kakobe kusema kuwa ana fedha nyingi kuliko Serikali, Mamlaka ya Mapato nchini TRA imejipanga kuanza kufuatilia ulipaji wake wa kodi. Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema mamlaka yake imeipokea kwa furaha kauli ya Askofu Kakobe na inataka kujiridhisha vyanzo vya utajiri huo. Kichere amesema TRA inafahamu kuwa shughuli za kidini hazitozwi kodi lakini inataka kufahamu kama fedha hizo za Askofu Kakobe zinatokana na sadaka pekee au kuna shughuli nyingine za kiuchumi. "Tumefuatilia hakuna kumbukumbu za Askofu Kakobe kulipa kodi, sasa tumeona tumfuate maofisa wetu wakajiridhishe kama fedha hizo anazozizungumzia zinatokana na sadaka," "Na kama hana shughuli zozote za kiuchumi ikiwa ina maana utajiri huo unatokana na sadaka ni jambo la kushtua kidogo lakini sisi tutaishia hapo," Amesema katika taarifa za mamlaka hiyo wapo watu wengi wenye fedha nyingi na k...

Agizo la Waziri Nchemba kama huna kitambulisho cha utaifa

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa Tanzania kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa kwani si zoezi la hiari na kwamba ni lazima kwa mtanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi ili kutambuliwa. Amesema hayo akizindua zoezi la kujiandikisha kupata kitambulisho  cha Taifa na kugawa vitambulisho katika Mkoa wa Ruvuma na kukagua zoezi hilo linaendaje kwa mikoa ya Nyanda za Kusini hasa iliyoko mipakani mwa nchi. Waziri Nchemba amewataka wananchi waache mazoea ya kutafuta kutambuliwa mpaka wanapokuwa na shida hasa za kutaka hati ya kusafiria au migogoro ya ardhi pale anapoambiwa yeye si raia wa Tanzania. Mh. Nchemba amewagiza viongozi wa wilaya na vijiji kutokuunganisha zoezi la kuandikisha wananchi kupata vitambulisho vya uraia na zoezi lingine lolote akitolea mfano baadhi ya viongozi kuchangisha fedha za kijiji kwa kuwaambia kuwa hutopata kitambulisho mpaka utakapo lipa fedha unazo daiwa na kijiji. "Hili zoezi...

LIBYA : MTOTO WA GADDAFI KUGOMBEA URAIS MWAKANI

Image
KUTOKA LIBYA Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi, anatarajia kugombea urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2018. Taarifa za Saif al-Islam kutaka kugombea nafasi hiyo ambayo baba yake alikuwa ameishikilia kwa muda wa miaka 42, ilitolewa na msemaji wa familia Basem Hashimi Soul. "Saif al-Islam atagombea urais kwenye uchaguzi ujao ambao unaweza ukafanyika katikati mmwa mwaka 2018,ana dhamira ya kuongeza ulinzi zaidi na utulivu kulingana na jografia ya Libya, kwa kushirikiana na makundi yote ya Libya, hivi karibuni anatarajia kuweka wazi tarahe ya kujitangaza rasmi kwenye vyombo vya habari", amesema msemaji Basem Hashimi Soul. Nchi ya Libya hivi karibuni imekuwa isiyo ya utulivu, kutokana na vurugu zinazoendelea, huku mtoto huyo wa Gaddafi akiwa na imani kubwa Umoja wa Mataifa utakubaliana nae katika kipindi hiki kigumu ambacho nchi hiyo kinaipitia, cha kutafuta utulivu. Saif al-Islam ni mtoto wa pili wa Muammar Gaddafi ambay...

ANC yapata mwenyekiti mpya, Mama Zuma ‘apigwa mtama’

Image
Chama cha African National Congress (ANC), Afrika Kusini kimemchagua Cyril Ramaphosa, kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho akimrithi Jacob Zuma. Ramaphosa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama tawala nchini Afrika Kusini ANC leo baada ya kufanyika uchaguzi. Makamu huyo wa  rais aliyeibuka mshindi alikuwa na upinzani mkali na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa  Zuma. Kulikuwa na  mvutano, hisia zikipanda, wajumbe wakipiga kelele kupinga taratibu za upigaji wa kura. Uwaniaji madaraka umeleta mvutano  wa kisiasa nchini humo  hali inayoleta hofu kuwa ANC inaweza kugawanyika kabla ya uchaguzi wa 2019. Ramaphosa ameibuka mshindi kwa kupata kura  2,440 huku mpinzani wake  Dlamini-Zuma akipata kura 2,261

RAISI MAGUFULI AWAONYA WANACHAMA CCM

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Dk John Magufuli ameendelea kusimamia azma yake ya kumaliza rushwa ndani ya chama hicho. Dk Magufuli ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano amesema CCM haitasita kutengua matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu iwapo itabainika rushwa imetumika. Akifungua mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma leo Jumatatu Desemba 18,2017 Rais Magufuli amesema chama hicho kimedhamiria kupambana na rushwa. Amewataka wajumbe wa mkutano kuchagua watu waaminifu na wenye mapenzi ya dhati na CCM. “Msichague watu kwa urafiki au kwa sababu ya rushwa, binafsi napenda nimshukuru mzee Kikwete (Jakaya) yeye hakuangalia rushwa nadhani angefanya hivyo huenda mimi nisingepita,” amesema. Rais Magufuli amewataka wanachama wa CCM kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa chaguzi wa ndani wa chama hicho ulioanza Aprili, 2017. “Vunjeni makundi chaguzi zimekiwasha tujikite kwenye kukiimarisha chama. CCM haitamvumilia mtu mwenye kuendeleza ...

Chama cha ANC cha Afrika Kusini kumchagua kiongozi mpya

Image
Chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini, kinatarajiwa kupiga kura kumchagua mrithi wa Rais Jacob Zuma kama kiongozi wake. Wagombea wakuu ni makamu wa rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa, na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa rais Zuma. Harakati hizo za kutafuta kiongozi zimezua mvutano chamani na kuna hofu kuwa huenda ANC kikagawanyika kabla ya uchaguzi wa mwaka 2019. Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma anasema mustakabali wa chama tawala African National Congress upo katika tishio. Alikuwa anazungumza katika mkutano wa kumchagua mtu atakayemrithi kama kiongozi wa chama hicho, Rais Zuma alizungumza kuhusu haja ya kuwa na umoja ndani ya ANC, kinachotishiwa na kumeguka. Mkutano huo ulichelewa kuanza kutokana na mizozo kuhusu nani anayestahili kuruhusiwa kupiga kura. Zuma amesema tuhuma kuwa serikali yake ilishinikizwa na maslahi ya wafanya biashara zitachunguzwa, Rais Jacob Zuma amekiongoza chama hicho kwa muongo mmoja sasa. Chama hi...

Chadema walia kuchezewa rafu na CCM Moshi

Image
Zoezi la upigaji wa kura katika kata nne za majimbo ya Hai na Moshi mjini leo Jumapili limefanyika kwa amani huku Chadema ikilalamika kuchezewa rafu na CCM kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi. Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Moshi mjini, Priscus Tarimo, amesema hawaelewi msingi wa malalamiko ya Chadema, wakati Jeshi la Polisi wajibu wake ni kudhibiti uhalifu. “Polisi wanachokifanya ni kudhibiti vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani. Polisi hawawezi kukaa kimya wakati vijana wa Chadema wanatishia amani. Lazima wakamatwe,” amesema. “Salama yao ni kupiga kura na kurudi nyumbani waache vyombo vifanye kazi yao. Uchaguzi unasimamia na sheria na kanuni na polisi wanasimamia ili zisimamiwe,” amesisitiza Tarimo. Katibu huyo amesema uchaguzi huo ulikwenda vizuri kwa vile vituo vilifunguliwa kwa wakati na wananchi walipiga kura kwa amani tofauti na Chadema walivyokuwa wakilalamika. Hata hivyo, Katibu wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Basil Lema amesema awali...

CCM yashinda kata nne Arumeru Mashariki

Image
  Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeshinda kata nne za Arumeru Mashari ambazo wagombea wa Chadema wamejitoa. Kata hizo na matokeo yake ni kama ifuatavyo, Makiba Samson Laizer (CCM) kura 2,029 na Joyce Martin (Chadema) kura 608. Kata ya Ambuleni, Jasephat Jackson (CCM) kura 2,057 na Dominick Mollel (Chadema) kura 1,201. Kata ya Leguruki Andason Sikawa (CCM) kura 3,023 na Daniel Mbise(Chadema) kura 287. Kata ya Maroroni, Yoha Kaaya (CCM) kura 3,568 na Asanterabi Mbise (Chadema) 1,201.

RAIS MUGABE AMFUTA KAZI MAKAMU WARAISI

Image
Emmerson Mnangagwa Taarifa kutoka Harare zinasema kwamba, Makamu wa rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amefutwa kazi. Bw. Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75, ameachishwa kazi kwa madai kuwa alionyesha tabia za kukosa uzalendo na uaminifu hasa kwa Rais.  Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari wa Zimbabwe Simon Kahaya Moyo. Kufutwa kwake ni ishara kuwa mke wa rais Robert Muabe, Bi Grace, atafuata nyayo za mumeme za kuwa rais wa Zimbabwe. Siku ya Jumapili Bi Grace Mugabe alitoa wito wa kutaka mumewe amfute kazi Mnangagwa. Bwana Mnangagwa, ambaye ni mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi, amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe. Kufutwa kwake kunakuja baada ya Rais Robert Mugabe, 93, kutishia kumuachisha kazi Bw Mnangagwa, hatua ambayo imezua uvumi kuwa anataka mke wake kuchukua hatamu za kuliongoza taifa hilo. Akihutubia mkutano wa wanachama wa makanisa ya asili mji Harare siku ya Jumapili, Bi Mugabe alisema: "Nyoka ni lazima apiwe kwenye ki...