UKIWA NA SIFA HIZI LAZIMA UOLEWE!
M OJA kati ya kilio kikubwa cha mabinti ni kupata wanaume sahihi wa kuwaoa. Ishu si tu kuolewa lakini kupata mume sahihi ni jambo lingine. Wengi wanaishia kukutana na wanaume ‘wasanii’ ambao hawana mpango wa ndoa. Wao wanafurahia maisha ya ujana hadi pale watakapojisikia. Kwa kuwa kiasili mwanaume ndio humfuata mwanamke, fursa ya kuanza kuchagua mke mtarajiwa, mchumba, ‘girlfriend’ huwa inaanza kwa mwanaume. Wazo la kukufanya wewe kuwa rafiki, mchumba na baadaye mke mara nyingi huwa linaanza kwa mwanaume. Hivyo basi utakubaliana na mimi kwamba, kwa kiasi kikubwa mwanaume ndio mwenye ‘funguo’ ya ndoa. Ndiye anayeweza kusema ‘Yes’ au ‘No’. Mara nyingi mwanaume ndiyo mwenye maamuzi ya kusema nioe au nisioe kwa sasa. Ndio mwenye uamuzi wa kusema nioe mwanamke huyu au nisimuoe nitaoa mwingine. Nimuoe huyu kwa sababu ananifaa, nimuache huyu kwa sababu hanifai. Licha ya kuwa mwanaume anaweza kuwa na matatizo yake lakini pamoja na yote hayo, jukumu la kufanya maamuzi huwa linaba...