MHARIRI ASEMA SAYANSI NA TEKNOLOJIA NI CHANGAMOTO KATIKA UCHAPISHAJI(MAENDELEO YA TEHAMA NA CHANGAMOTO ZAKE KATIKA UCHAPAJI)

Na HUGHOLIN KIMARO Masshele blog Kwa Mukhtasari Mhariri wa Kiswahili wa matbaa ya Longhorn Kenya, Bw James Mwilaria, amesema uchapishaji wa vitabu katika awamu hii ya utandawazi umekumbwa na changamoto tele ingawa upo uzuri wake pia. MHARIRI wa Kiswahili wa matbaa ya Longhorn Kenya, Bw James Mwilaria, Alhamisi aliwaelezea wataalamu, wasomi na wapenzi wa Kiswahili kwamba uchapishaji wa vitabu katika awamu hii ya utandawazi umekumbwa na changamoto tele ingawa upo uzuri wake pia. Kulingana na Bw Mwilaria, ingawa uchapishaji wakati huu wa utandawazi ni rahisi, unakabiliwa na changamoto si haba. “Waandishi na wachapishaji wamekuwa wakichangamkia sana uchapishaji wa kidijitaji bila kujua kuwa unazo changamoto zake. Wenyewe ni rahisi kwani hata baadhi ya waandishi wamekuwa wakijiandikia na kujichapishia miswada. Lakini mambo si shwari kama inavyofikiriwa. Kuna tatizo la kudhibiti hakimiliki za wachapishaji. Unapochapisha vitabu katika enzi hizi inakuwa vigumu kui...