Posts

Showing posts with the label fonimu za kiswahili

fonimu na muundo wa silabi za kiswahili

 Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili 10 Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili Benard Odoyo Okal Ikisiri Fonimu ni kipashio kidogo cha sauti ya lugha chenye uwezo wa kubainisha maana na hudhihirika kama irabu au konsonanti. Kama ilivyo katika lugha nyinginezo ulimwenguni, Kiswahili vilevile kina fonimu za kategoria mbili yaani irabu na konsonanti. Hata hivyo, idadi ya fonimu konsonanti za Kiswahili inaelekea kuainishwa tofautitofauti kwa mujibu wa wanaisimu mbalimbali wa Kiswahili. Mathalani, wanaisimu wengine wanadokeza idadi ya fonimu konsonanti kuwa 24, 25, 26, 29, 32 au 33. Kwa upande mwingine, miundo ya silabi za Kiswahili pia hudokezwa kuwa tofauti kama vile 4, 5, 6, 7 na 8. Idadi tofauti ya fonimu konsonanti za Kiswahili pamoja na idadi tofauti ya miundo ya silabi za Kiswahili huelekea kuwakanganya wasomaji wa lugha ya Kiswahili. Hivyo basi, makala hii inalenga kuhakiki fonimu na miundo mbalimbali ya silabi za Kiswahili. Ili kufanikisha uhakiki huu...

kubainisha fonimu

  Jambo moja ambalo limejitokeza katika yale tuliyoyasema kuhusu uanishaji wa fbnimu na alofbni ni umuhimu wa mfanano wa sifa za kifonetiki kati ya sauti tulizotolea mifano. Kwa mfano, tumeona kuwa sauti [t] na [d] zinatofautiana katika sifa moja tu, ya  ughuna,  zinachangia sifa za mahali pa kutamkia (zote ni za ufizi), na namna ya utamkaji (zote ni vipasuo). Hali kadhalika [t] na [th] zinatofautiana katika sifa moja tu, ya  mpwnuo;  zinachangia sifa za mahali pa kutamkia (zote ni za ufizi), na namna za utamkaji (zote ni vipasuo, na zote ni sigbuna). Katika kuchunguza mifumo-sauti ya lugha mbalimbali, mfanano wa kifonetiki kati ya sauti ni muhimu sana, kwa vile mahusiano yote ya kifonolojia, kanuni, pamoja na minyumbuo yote, kama tutakavyoona, yanaegemea katika sifa hii. Katika kuainisba sauti za lugha ili kugundua zipi ni fonimu za lugha biyo pamoja na alofoni zao, umuhimu huwekwa katika kuangalia uhusiano uliopo kati ya makundi ya sauti kufuatana na mahali pa...