Jambo moja ambalo limejitokeza katika yale tuliyoyasema kuhusu uanishaji wa fbnimu na alofbni ni umuhimu wa mfanano wa sifa za kifonetiki kati ya sauti tulizotolea mifano. Kwa mfano, tumeona kuwa sauti [t] na [d] zinatofautiana katika sifa moja tu, ya ughuna, zinachangia sifa za mahali pa kutamkia (zote ni za ufizi), na namna ya utamkaji (zote ni vipasuo). Hali kadhalika [t] na [th] zinatofautiana katika sifa moja tu, ya mpwnuo; zinachangia sifa za mahali pa kutamkia (zote ni za ufizi), na namna za utamkaji (zote ni vipasuo, na zote ni sigbuna).

Katika kuchunguza mifumo-sauti ya lugha mbalimbali, mfanano wa kifonetiki kati ya sauti ni muhimu sana, kwa vile mahusiano yote ya kifonolojia, kanuni, pamoja na minyumbuo yote, kama tutakavyoona, yanaegemea katika sifa hii. Katika kuainisba sauti za lugha ili kugundua zipi ni fonimu za lugha biyo pamoja na alofoni zao, umuhimu huwekwa katika kuangalia uhusiano uliopo kati ya makundi ya sauti kufuatana na mahali pa kutamkia, na namna za utamkaji. Makundi makubwa yanayohusiana sana ni matatu: vipasuo, vikwamizi, na ving’ong’o.

Ndani ya makundi haya, umuhimu mkubwa unawekwa katika mahali pa kutamkia. Sifa nyingine za jinsi ya kutamka, kama ughuna na mpumuo, kwa kawaida bazitangui uhusiano huu, bali huuchonga zaidi. Kwa mfano, kati ya lugha ambazo zimechunguzwa, hakuna ambayo imeonekana kuwa na sauti [t] (ya ufizi) na [k] (ya kaakaa laini) zikawa alofoni za fonimu moja; ingawa zote ni vipasuo, na zote ni sighuna, kwa sababu zinatofautiana sana katika mahali pa kutamkia. Lakini ni kawaida katika lugha nyingi kukuta kuwa sauti [t] (ya ufizi, sighuna) na [dj (ya ufizi, ghuna) ni alofoni za fonimu moja; halikadhalika [k] (ya kaakaa laini, sighuna) na [g] (ya kaakaa laini, ghuna).

Kati ya makundi mengine, uhusiano unaweza kujitokeza kwa namna tofauti. Kwa mfano, mara nyingi kati ya vikwamizi, uhusiano si kati ya sauti gbuna na sighuna tu, bali pia kati ya sauti ambazo ziko karibu karibu katika mahali pa kutamkia. Hivyo inawezekana katika lugha fulani, sauti [q] na [s] zikawa ni alofoni za fonimu moja, halikadhalika [d] na [z]. Sauti hizi, katika kilajozi, zinatamkiwa mahali tofauti: [q] na [d] ni za meno, ambapo [s] na [z] ni za ufizi; lakini zimekaribiana sana na zinawiana katika ughuna au usighuna.

Ving ‘ong ‘o mara nyingi pia vinakuwa na uhusiano wa kialofoni, kwa mfano, [m] na [nj zinaweza kuwa alofoni za fonimu moja.

Uhusiano unaweza kujitokeza vile vile kati ya sauti ambazo ziko katika makundi tofauti lakini zinachangia mahali pa kutamkia. Kwa mfano kipasuo cba meno sighuna [þ] na kikwamizi cha meno sighuna [q] zinaweza kuwa alofoni za fonimu moja. Ikitokea hivyo, ni kawaida katika lugha hiyo hiyo sauti zinazohusiana na hizo kuwa alofoni za fonimu moja, yaani kipasuo cha meno ghuna [d] na kikwamizi cha meno ghuna [d].

Lakini, hata kama tunajua ni sauti zipi zinaweza kuhusiana katika lugha fulani, hatuwezi kujua kwa uhakika zipi ni fonimu katika lugha hiyo bila kuwa na vigezo halisi. Kigezo kimoja muhimu, na ambacho tumekuwa tunakitumia mpaka sasa ni jozi za maneno ambayo yanatofautiana katika sauti moja tu. Hivyo maneno yafuatayo ya Kiswahili

8 a) {dua} na
b) {tua}

yanatofautiana katika kuwepo kwa [t] mahali pa [d]. Sauti zote nyingine zinabaki zilivyo, na mazingira zinapotokea yanabaki yale yale. Mzungumzaji yoyote wa Kiswahili anajua kuwa maneno bayo mawili ni tofauti na hakuna mahali ambapo anaweza kuyachanganya. Na ndiyo sababu tunasema kuwa /d/ na /t/ ni fonimu tofauti katika Kiswahili. Jozi za maneno za namna hii zinaitwa jozi sahili. Hiki ni kigezo muhimu sana wanachotumia wanafonolojia katika kutambua sauti zipi ni fonimu katika lugha inayochunguzwa. Kigezo hiki kinawasaidia wachunguzi kuainisha sauti ambazo zina uhusiano wa karibu wa kifonetiki, na ambazo mchunguzi anahisi kuwa zinaweza kuwa na uhusiano wa kialofoni. Kwa mfano, baada ya kuhakikisha kuwa /d/ na /t/ ni fonimu tofauti za Kiswahili, mchunguzi anaweza kutumia kigezo hicho hicho cha jozi sahili kuhakikisha ikiwa sauti nyingine za vipasuo vyenye uhusiano wa ughuna na usighuna pia ni fonimu tofauti. Jozi za maneno yafuatayo zinamsaidia kufikia uamuzi:-

9 a){bana}
b) {pana}

10 a) {guna}
b) {kuna}.

Kwa vile maneno hayo ni tofauti, mchunguzi anahitimisha kuwa sauti /b,p,g,k/ ni fonimu tofauti katika Kiswahili. Mchunguzi anaweza kuendelea kufanya hivyo kwa sauti za makundi mengine. Jozi za maneno kama hizi zifuatazo zinampa uhakika wa mahitimisho yake:

11 a) {zaa} : {saa};
b) {vua} : {fua};
c) {saba} : {shaba}
d) {zana} : {dhana}; n.k.

Haya yanathibitisha kuwa sauti zifuatazo ni fonimu za Kiswahili: /z, s, v, f, Å¡, d/.

Ingawa jozi sahili ni kigezo muhimu, si mara zote, katika uchunguzi wa lugha fulani, inawezekana kupata jozi hizo katika kupima sauti zote tunazozitilia mashaka. Tuseme kwa mfano kuwa katika Kiswahili tunajua kuwa kuna maneno yenye sauti [l] na mengine yenye sauti [r] ambazo zote ni vilainisho, lakini hatuwezi kupatajozi sahili zitakazotuthibitishia kuwa hizi ni fonimu tofauti. Hapa itabidi tutumie hisia za wazungumzaji. Ikiwa mzungumzaji mmoja atasema {mtoto anaria} na wenzake haraka wakamsahihisha ‘hatusemi anaria, tunasema analia’, hapo mchunguzi atajua mara moja kuwa sauti hizi ni tofauti hata kama hakunajozi sahili, ikiwa wazungumzaji wanasisitiza kuwa hazifanani. Baadaye, anaweza kugundua maneno kama {kula} na {kura} ambayo yatampa uhakika zaidi. Kigezo kingine ni kuangalia, pamoja na hisia za wazungumzaji, mazingira katika neno ambapo sauti zinazochunguzwa zinatokea. Kwa mfano, sauti zote mbili [l] na [r] zinatokea katika mazingira yanayofanana:-

12 a) Mwanzo: {raha: lala}
b) Kati: {kibali: kiburi}
c) Baada ya konsonanti: {mrpho: mlango}.

Mbinu hii ni muhimu kwa sababu, kwa kawaida sauti ambazo ni fonimu tofauti zinaingiliana katika mazingira zinamoweza kutokea katika neno, yaani moja inapoweza kutokea, na nyingine inaweza kutokea. Mifano iliyotolewa katika sehemu hii inadhihirisha hoja hii. Tutaona katika sehemu inayofuata kuwa uhusiano huu ni tofauti na ule wa alofoni za fonimu moja