Posts

Showing posts with the label michezo na burudani

KUTOKA SHINYANGA: HALI YA BOKO ILIVYO HIVI SASA

Image
Nahodha wa Simba, John Bocco atafanyiwa vipimo leo asubuhi mjini Shinyanga ili kujua amepata maumivu kwa kiasi gani. Hali hiyo inatokana na Bocco kuumia jana ikiwa ni dakika chache baada ya kuifungia Simba bao dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Bocco alitolewa nje baada ya kushindwa kuendelea na kitengo cha tiba cha Simba, kimeeleza kwamba atafanyiwa vipimo hivyo ili kujua tatizo hilo kwa undani zaidi. Baada ya ya vipimo hivyo, suala litakalofuatia ni matibabu ili kuhakikisha anarejea katika hali yake                              TANGAZO

Umekiona kikosi cha simba Leo?

Image
KIKOSI CHA SIMBA LEO VS MWADUI FC 1. Aishi Manula 2. Shomari Kapombe 3. Mohammed Hussein 4. Juuko Murshid 5. Yusuf Mlipili 6. Erasto Nyoni 7. Shiza Kichuya 8. Said Ndemla 9. John Bocco 10. Emmanuel Okwi 11. James Kotei SUB: Emmanuel Mseja Ally Shomari Peter Bukaba Nicholas Gyan Mzamiru Yassin Mwinyi Kazimoto Laudit Mavugo                              T

RONALDO APIGA HATRICK SOCIEDAD WAKILALA 5_2

Image
Real Madrid: Navas, Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo; Vazquez (Isco 63), Modric (Kovacic 63), Kroos, Asensio (Bale 73); Benzema, Ronaldo Subs not used: Nacho, Casilla, Hakimi, Casemiro Goals: Vazquez 1, Ronaldo 27, 37, 80, Kroos 34 Yellow cards: Carvajal, Kovacic Real Sociedad: Rulli, Odriozola, Elustondo, Navas, De La Bella; Canales (Bautista 60), Illarramendi, Zurutuza (Zubeldia 60); Oyarzabal, Xabi Prieto, Juanmi (Guridi 83) Subs not used: Llorente, Agirretxe, Ramirez Martinez, Rodrigues Goals: Bautista 74, Illarramendi 83 Yellow cards: De La Bella 

MSUVA APIGA HATRICK TIMU YAKE IKISHINDA 10--0

Image
Mtanzania Saimon Msuva amepiga hat trick timu yake ya Difaa Al Jadid ikishinda kwa mabao 10-0 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Benfica Bissau ya Guinea Bissau. Mechi hiyo ambayo Jadid walikuwa nyumbani, Msuva amefunga mabao hayo matatu mshambuliaji mwingine Ahaddah Hamed akifunga matano. Ndiaye na El Magri nao walifunga mabao mengine na kukamilisha mauaji hayo ya shelabela ya Al Jadid. Mtanzania huyo alionyesha soka safi ikiwa ni pamoja na kutengeneza mabao ya wenzake. Msuva aliyejiunga na timu hiyo akitokea Yanga, alifunga mabao hayo katika dakika za 45, 73 na lile la kukamilisha 10 dakika ya 87.

SIMBA NDIYE BINGWA MPYA VPL 2017/2018 SABABU HIZI HAPA

Image
Na Masshele Emanuel SIMBA imefanikiwa kushinda mechi nne mfululizo kwa idadi kubwa ya mabao ambayo yanaifanya kuwa timu hatari zaidi katika kipindi hiki unapozungumzia Ligi Kuu Bara. Katika mechi nne, Simba imekusanya pointi 12, maana yake imeshinda bila ya kupotea hata moja, jambo ambalo linaonyesha mwendo wao ni mzuri zaidi. Lakini utaona katika mechi zote nne, Simba imeshinda mabao 2-0 katika mechi mbili na 4-0 katika mechi mbili. Hawajaruhusu hata bao moja kutinga katika nyavu zao. Katika ligi kama ya sasa ambayo ugumu wake unajulikana, timu kucheza mechi nne na kufunga mabao 12, si jambo dogo. Lakini timu kucheza mechi nne bila ya kuruhusu hata bao moja, maana yake ni kiwango bora kabisa cha utendaji kwa maana ya ulinzi na ushambulizi. Mechi tatu za mwanzo, Simba iliifunga Ndanda FC kwa mabao 2-0 ikiwa ugenini, ikaitwanga Singida United 4-0 jijini Dar es Salaam na kusafiri kwenda Bukoba ambako waliivurumisha Kagera Sugar 2-0. Hapa kikosi kilikuwa chini ya ...

Manula aweka rekodi ya kutofungwa Simba

Image
Golikipa wa vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC Aishi Manula amefanikiwa kujiwekea rekodi ya pekee tangu ajiunge na klabu hiyo mwezi Juni 2017 akitokea Azam FC. Manula ameichezea Simba mechi 20 ambapo kati ya hizo mechi 14 hajaruhusu lango lake kufungwa hata bao moja hivyo kuwa msaada mkubwa kwa kikosi hicho kinachoongoza ligi kwa alama 35. Katika rekodi hiyo ya Manula  mechi za kukumbukwa zaidi ni mechi yake ya kwanza ndani ya Simba ambayo ilikuwa siku ya Simba Day dhidi ya Rayol Sports ya Rwanda. Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0. Mechi nyingine ni ile dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani ambayo ilikuwa ni mechi yake pili kwake na timu hizo zilitoka sare ya 0-0 katika dakika 90. Mechi ya kwanza ya ligi kwa Manula akiwa na Simba ilikuwa ni ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting. Mechi nyingine ambazo zimebaki kama alama ya uwezo wa Manula ndani ya Simba ni mechi tatu za mwisho kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi, Simba ikishinda 4-0 dhidi ya Singid...

Tambwe kuivaa Azam FC kesho?

Image
  Straika wa Yanga, Amissi Tambwe raia wa Burundi ameshindwa kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake kutokana na majeraha ya goti. Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu arejee na acheze mechi dhidi ya Mwadui FC kabla ya kuwavaa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar. Mshambuliaji huyo akiwa amekaa nje ya uwanja huku wenzake wakiendelea na mazoezi. Mshambuliaji huyo, alipata majeraha hayo juzi Jumatano katika mazoezi ya timu hiyo baada ya kugongana na beki wa pembeni, Juma Abdul na kushindwa kuendelea na programu nyingine. Kutokana na Tambwe kushindwa kufanya mazoezi ya mwishoni ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo, upo uwezekano wa Mrundi huyo kuikosa mechi dhidi ya Azam FC. Katika mazoezi hayo ya jana, benchi la ufundi la timu hilo, lilionekana kuwaandaa baadhi ya washambuliaji watakaocheza nafasi yake ambao ni Juma Mahadhi na Yohana Nkomola.

Simba kujichimbia tena Morogoro

Image
KIKOSI cha Simba kinatarajia kwenda tena Morogoro au Zanzibar kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuwavaa wapinzani wao katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, klabu ya Gendarmarie Nationale kutoka Djibouti, imefahamika. Vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ambao wanadhaminiwa na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa wanatarajia kuwakaribisha Gendarmarie katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Februari 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Akizungumza na gazeti hili jana, Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah "Try Again" alisema jana kuwa uamuzi kamili utafanywa katika kikao cha pamoja na benchi la ufundi baada ya kumaliza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Majimaji itakayofanyika Jumapili. Salim alisema uongozi wa klabu hiyo unaamini kuwa kambi hiyo watakayokaa itasaidia kuwaweka wachezaji tayari kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo wao wa kwanza wa kimataifa ambao utakuwa ni m...

Former Gor Mahia midfielder joins KCB

Image
Former Gor Mahia midfieler Erick 'Cantona' Ochieng has joined National Super League (NSL) side KCB on a one-year deal . The veteran midfielder has been out of action since June 2017 when he parted ways with Kenyan Premier League side, Nakumatt. Promotion He is now back to action with Kenya Commercial Bank (KCB) FC that will be looking to earn promotion to the Kenyan Premier League this season after narrowly missing out in 2017. The club has also appointed John Kamau as head coach and the former Thika United, Posta Rangers and FC Talanta boss will be hoping for a strong start to 2018 season.

KOCHA WA MWADUI AANGUKA BAFUNI NA KUFARIKI DUNIA SHINYANGA LEO

Image
Na Mwandishi Wetu, MWADUI KOCHA Msaidizi wa Mwadui FC, Jumanne Ntambi  (pichani kulia)  amefariki dunia usiku wa leo baada ya kuanguka bafuni wakati anaoga nyumbani kwake Mwadui mkoani Shinyanga. Taarifa za awali zinasema mwalimu Ntambi baada ya kuanguka bafuni alikimbizwa hospitali ambako walikofika, wakasema tayari amekwishafariki dunia. Imeelezwa Ntambi alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu na jana alikwenda hospitali kwa matibabu akaambiwa apumzike, ingawa leo aliwatembelea wachezaji mazoezini Uwanja wa Mwadui Complex. Mmoja wa wachezaji wa Mwadui FC, Athumani Maulid ameiambia masshele –Blog usiku huu kwamba; “Tumepata msiba, kocha wetu Ntambi amefariki dunia usiku huu”. Maulid mmoja wa wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys ya mwaka jana ameongeza; “Kocha alikuwa anaumwa na leo hakuja mazoezini kikazi. Alikuja tumekwishamaliza akatusalimia, tukazungumza naye, akaondoka ndipo baadaye zikaja taarifa za kifo chake,”am...

NYOSO HAJAACHA UJINGA AMEFANYA TUKIO HILI LEO BAADA YA TIMU YAKE KUPOTEZA 2-0

Image
  Juma Nyoso akiwa chini ya Ulinzi wa polisi Baada ya pambano kati ya Kagera Sugar na Simba kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabai 2-0, beki wa Kagera Sugar Juma Nyoso amemshambulia shabiki na kumpiga hadi kuzimia.  Nyoso anashikiliwa na Polisi huku shabiki huyo akipatiwa matibabu hospitali   Shabiki aliyepigwa akipatiwa huduma ya kwanza

UTAMU WA LIGIKUU KUREJEA IJUMAA( VPL) HII HAPA RATIBA YAMECHIZOTE

Image
  Ligi Kuu soka Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea Ijumaa, Disemba 29 baada ya mapumziko ya takribani wiki tatu kupisha michuano inayosimamiwa na baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati 'CECAFA Challenge' iliyomalizika nchini Kenya wiki iliyopita kwa wenyeji, Harambee Stars kuwa mabingwa wakiwafunga Zanzibar katika fainali. Ratiba inaonesha kuwa siku hiyo ya Ijumaa, kutakuwa na mchezo mmoja kwa mabingwa mara moja wa taji hilo Azam FC ‘Wanarambaramba’ kuwa wenyeji wa Stand United ‘Chama la Wana’ mchezo ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 usiku. Jumamosi kutakuwa na michezo mitatu, Lipuli FC ‘Wanapaluhengo watacheza na na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Samora, Iringa kuanzia Saa 8:00 mchana, huku Mtibwa Sugar na Maji Maji wakicheza kwenye uwanja Uwanja wa Manungu complex, Turiani, Morogoro. Mchezo wa Tatu siku hiyo  Ndanda FC ‘Wanakuchele’ watakuwa na kibarua kizito pale watakapomkaribisha ...

RATIBA YA KOMBE LASHIRIKISHO

Image
RATIBA YA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM SPORTS HII HAPA..

Mohamed Ibrahim amemalizana na simba

Na mwandishi wetu Klabu ya Simba imemalizana na mchezaji wake Mohamed Ibrahim na kukubaliana kumuongezea mkataba. Ibrahim maarufu kama Mo Ibrahim, alitarajia kuongeza mkataba leo mchana. “Ilikuwa ni leo mchana, sijajua imekuwaje lakini kila kitu kimemalizika na makubaliano ya kila kitu yameenda vizuri. “Suala la kusaini mkataba ndiyo lilibaki na sasa hakuna hofu tena,” kilieleza chanzo. Kumekuwa na taarifa kwamba, Mo Ibrahim anaweza kuondoka Simba, ikiwa ni baada ya mkataba wake kwisha.

Kombe la Dunia Urusi 2018: Utaratibu wa kufanyika kwa droo

Image
Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Droo ya Kombe la Dunia 2018 itafanyika katika ukumbi wa State Kremlin Palace Ijumaa, 1 Desemba Mataifa ambayo yamefuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Urusi mwaka ujao yatafahamu yatakutana na nani hatua ya makundi droo itakapofanyika leo Urusi. Kombe hilo la Dunia litashirikisha timu 32, na michezo itachezwa kati ya 14 Juni na 15 Julai. Afrika inawakilishwa na Misri, Nigeria, Morocco, Tunisia na Senegal. Mataifa yaliyofuzu Kupangwa kwenye vyungu Kuelekea zoezi hilo baadhi ya timu zimepangwa kwenye vyungu, chungu cha kwanza ambacho kina timu mwenyeji Urusi, Ujerumani, Brazil, Ureno, Argentina, Ubelgiji, Poland na Ufaransa. Vyungu vimepangwa vipi? Vyungu Kombe la Dunia Chungu 1 Chungu 2 Chungu 3 Chungu 4 Urusi (wenyeji) Uhispania (8) Denmark (19) Serbia (38) Ujerumani (1) Peru (10) Iceland (21) Nigeria (41) Brazil (2) Uswizi (11) Costa Rica (22) Australia (43) Ureno (3) England ...