MSUVA APIGA HATRICK TIMU YAKE IKISHINDA 10--0




Mtanzania Saimon Msuva amepiga hat trick timu yake ya Difaa Al Jadid ikishinda kwa mabao 10-0 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Benfica Bissau ya Guinea Bissau.


Mechi hiyo ambayo Jadid walikuwa nyumbani, Msuva amefunga mabao hayo matatu mshambuliaji mwingine Ahaddah Hamed akifunga matano.

Ndiaye na El Magri nao walifunga mabao mengine na kukamilisha mauaji hayo ya shelabela ya Al Jadid.

Mtanzania huyo alionyesha soka safi ikiwa ni pamoja na kutengeneza mabao ya wenzake.

Msuva aliyejiunga na timu hiyo akitokea Yanga, alifunga mabao hayo katika dakika za 45, 73 na lile la kukamilisha 10 dakika ya 87.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?