Posts

Showing posts with the label Umuhimu wa fonetiki

Umuhimu wa fonetiki

Yaliyomo 1. Umuhimu wa fonetiki   Kati ya matawi hayo matatu, Fonetiki-tamshi ndilo tawi ambalo limechunguzwa kwa undani zaidi na kwa muda mrefu sana (hasa kutokana na changamoto iliyotokana na kugundulika kwa sarufi ya Sanskrit na wanazuoni wa nchi za Ulaya Magharibi katika kame ya kumi na nane, kama tulivyosema hapo mwanzo). Istilahi nyingi za kifonetiki zinazotumiwa na wanaisimu zinahusiana na tawi hili. Katika sura hii, hili ndilo tawi ambalo tutaliangalia. Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa katika Fonetiki-safirishi umesaidia sana katika kutia nguvu baadhi ya mahitimisho yaliyofikiwa na wataalamu wa Fonetiki-tamshi. Kwa mfano:- i) imethibitika kuwa kila sauti inayotolewa na kiungo-sauti cha mwanadamu ni tofauti na nyingine kwa kiasi fulani. Hivyo sifa bainifu zinazotolewa kuhusu  foni  (kama tutakavyoona hivi punde) ni za wastani, na kuna mambo mengi ambayo yanaachwa, mambo ambayo mwanafonetiki anaona kuwa hayasaidii katika kufanikisha mawasiliano kati ya wajua-lugba. ...