Maneno 100 Ya Kumwambia Mwanamke Ili Moyo Wake Usisimke

Orodha ya maneno 100 ya kumsisimua mpenzi wako (Sms 100 za mapenzi za kumtumia mpenzi wako) Hivi yule mwanamke unayemtongoza ushamwambia maneno mangapi matamu na akakuambia kwa upole, “Nakupenda mpenzi wangu”. Iwapo hujawahi kutamkiwa maneno kama haya na mwanamke kwa njia ya upole basi itakuwa yale maneno unayomwambia hayatosheki. Mwanamke anapenda kuona kuwa unamfukuzia. Anataka kujua iwapo unamwona ni mrembo na kuvutia au la. Wanawake ni viumbe tofauti na huchagua maneno. Unaweza kuwa kila siku unamrushia mistari ama voko ambazo umekuwa ukizihifadhi kumbe kwake haoni chochote. Kabla hatujaendelea, sababu ya kuandika post hii ni kuwa kuna rafiki yangu katika mtandao wa Facebook amekuwa akiniandama akitaka nimpe mistari angalau mmoja ili aweze kumzuzua mpenzi wake. Well, kwa hili tulikaa na paneli yetu na tukaamua kuweka maneno 100 ambayo bila shaka yatamridhisha mwanamke yeyote. Zama nasi. Maneno matamu ya kumwambia mwanamke Nakumbuka ile siku ya kwanza ambayo macho y...