UHAKIKI RIWAYA YA FIRAUNI SEHEMU YA TATU
Firauni ni riwaya mpya iliyotoka hivi karibuni. Upya wa riwaya hii si tu kwa sababu imechapishwa hivi karibuni, la hasha! Bali ni kwa sababu ya upya wa mawazo yake ambayo yanasawiri barabara matukio anuwai yatokeayo katika jamii zetu wakati huu. Riwaya hii iliandikwa na mpenzi wa Kiswahili Athumani Mauya inatugusa sisi Watanzania na pia watu wa jamii nyingine za Kiafrika kwa sababu ya uhalisia na uzito wa matukio yanayojadiliwa na mwandishi huyu Athumani Mauya. Akiwa Dar es Salaam alikutana na msichana mrembo aliyejulikana kwa jina la Kunguru ambaye alikuwa amelelewa na katika maadili, mpole, mwenye heshima na adabu, mkweli asiye na hatia. Buna aliamua kumuoa binti huyo. Wakati wa kupima afya zao kabla ya kuoana Buna alikula njama na daktari ili majibu ya damu yatoke kwa matakwa ya mashine. Buna laifariki dunia kwa Ukimwi akiwa mikononi mwa Kunguru na kumwacha na msongo wa...