Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Tano AWAMU YA TATU TAARIFA KWA UMMA Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano Awamu ya Tatu mwaka 2017 wataanza masomo yao tarehe 21 Novemba, 2017 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 4 Desemba 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, atakuwa amepoteza nafasi. Mwanafunzi mara uonapo jina lako kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwamba umechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, inabidi ku-download fomu ya kujiunga na shule husika kwenye mtandao. Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano Awamu ya Tatu mwaka mwaka 2017 pamoja na fomu za kujiunga na shule (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz Imetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Tafadhali bofya chini Kuj...