Formfive selections
Vigezo vya kujiunga Na kidato cha tano 2023

Baada ya Matokeo ya kidato channel kutangazwa wanafunzi wengi wamekuwa wakijiuliza Je ni vigezo vipi vitatumika katika selection za kidato cha tano 2023?

Vigezo vinavyotumika katika miaka yote katika uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha tano ni hivi hapa

-Awe amesoma angalau masomo 7 nakuyafanyia mtihani.

-Awe umepata  division 1 hadi division 3

-awe amefaulu masomo matatu kwa kiwango cha credit yani A-C, Na ufaulu huo usihusishe masomo ya dini.

-katika masomo aliyofaulu yawe Na uwezo wakuumba combination/taasusi isiyozidi salama kumi(10) A=1 B=2, C=3 , D=4 F=5

Mfano alipata Chem A, Bios B phy C A+B+C = 6

-Kwenye combination aliyoichagua kusiwe Na somo lenye F.


-Awe alijaza selfom kwaajili ya kuchagua kujiunga Na kidato cha tano. Wengine huchagua kujiunga Na vyuo.

-Awe Na umri usiozidi miaka 25

 NB kwa kawaida wale waliofaulu sana kulingana Na taasusi walizozichagua hupewa kipaumbele. Lakini pia serikali hujitahidi kadri iwezavyo kuhakikisha hakuna mwanafunzi mwenye  sifa atakayeachwa.