Posts

Showing posts with the label UDOM

Taarifa muhimu kwa wanafunzi wa vyuo kutoka Bodi ya Mikopo (HESLB)

Image
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawataarifu wanafunzi wanaonufaika na mikopo kuwa  wanatakiwa kuendelea kuingiza taarifa zao kwa njia ya mtandao kupitia http://olas.heslb.go.tz   hadi tarehe 31 Januari, 2018. Wanafunzi wanufaika wanapaswa kufanya yafuatayo: •    Tembelea mtandao wa http://olas.heslb.go.tz •  Fungua kiunganishi cha “Click here to start” kwenye maelezo ya mwanzo ya kukaribisha. •    Weka namba yako ya mtihani ya Kidato cha Nne na mwaka uliofanya mtihani huo, kwa mfano: S0129.0004.2020 •   Weka namba yako ya akaunti ya Benki kama ilivyowasilishwa HESLB au kama inavyoonekana kwenye “signing sheet” •    Ingiza neno jipya la siri na ulithibitishe. •   Baada ya kuthibitisha, ukurasa wa kuweka picha yako “passport size photo” utafunguka. •    Weka picha yako ya rangi katika ukubwa wa 120×150 •    Wanufaika wapya wa mikopo kwa mwaka wa masomo 201...

Wanafunzi 12,000 wachaguliwa kujiunga Udom

Image
Dodoma. Baada ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kuacha kuwapangia vyuo wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimepata ongezeko la wanafunzi kutoka 4,500 hadi 12,000 kwa mwaka wa masomo wa 2017/2018. TCU imeacha kuwapangia wanafunzi vyuo kutokana na agizo lililotolewa na Rais John Magufuli mwaka huu, alipozindua mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Ofisa Uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazar amesema jana Jumanne Oktoba 31,2017 kuwa, katika mwaka wa masomo wa 2016/17 walipata wanafunzi 4,500 kutoka TCU. Amesema mwaka huu wa masomo wamepata maombi ya wanafunzi 43,000 na waliochaguliwa ni 12,000 ambao wamekidhi vigezo. Amesema ili kudhibiti tatizo la msongamano wa wanafunzi wanaosajiliwa chuoni hapo wameboresha utaratibu kwa kuongeza watumishi wanaowasajili na huduma za benki kusogezwa chuoni. Ofisa huyo amesema Benki ya CRDB inatoa huduma kwa kutumia tawi linalohamishika na kuwa na mawakala, hivyo wanafunzi hufungua akaunti chuoni badala ya kwenda mjini. Meneja wa Taw...