Posts

Showing posts with the label uhakiki

UHAKIKI WA RIWAYA YA ADILI NA NDUGUZE

  UCHAMBUZI WA FANI NA MAUDHUI KATIKA RIWAYA YA “ADILI NA NDUGUZE” ILIYOANDIKWA NA SHAABAN ROBERT 1.0   Utangulizi Kazi hii inahusu uchambuzi wa fani na maudhui katika riwaya ya “Adili na Nduguze ” iliyoandikwa na Shaban Robert mwaka 1952. Katika kujadili riwaya hii tutaeleza dhana ya riwaya, usuli wa mwandishi, muhtasari wa kitabu chenyewe, nadharia zitakazotumika kuchambua fani na maudhui ya kitabu hiki, uchambuzi wa fani na maudhui na hitimisho.   1.1 Dhana ya Riwaya Kwa mujibu wa Madumulla (2009) akimrejelea Msokile (1992) anafafanua kuwa riwaya ni kazi ya sanaa ya kubuni, ni maandishi ya nathari (ujazo) yanayosimulia hadithi ambayo kwa kawaida ina uzito, upana, urefu wa kutosha, ina wahusika wengi wenye tabia mbalimbali, ina migogoro mingi mikubwa na midogo.   Senkoro (1982) anasema riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja, na yenye mazungumzo na maelezo yanayozingatia kwa undani na upana maisha ya jamii. ...