Wanafunzi 26,688 kukosa mikopo elimu ya juu 2021-22

Hiyo ni sawa na asilimia 30.1 ya waombaji wote. Serikali yatenga mikopo ya Sh570 bilioni kwa wanafunzi 162,000. Majina ya waliopata mikopo kuwa wazi kabla ya Oktoba 25. Dar es Salaam. Wakati Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ikijiandaa kuwapangia wanafunzi wa elimu ya juu mikopo yao mwezi huu, wanafunzi wa 26,688 walioomba mikopo hiyo kwa mwaka 2021/22 hawataweza kupata mikopo hiyo. Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo HESLB, Dk Veronica Nyahende amesema majina ya wanafunzi waliopata mikopo wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu mwaka 2021/22 yatatangazwa mapema kabla ya vyuo kufunguliwa kuanzia Oktoba 25 mwaka huu. Hadi kufikia Septemba 30, HESLB ilikuwa imepokea maombi 88,688 na kati ya maombi hayo; 85,706 yalikuwa kamilifu na kutoa siku nne kuanzia Oktoba 4 hadi 7 kwa maombi yenye kasoro kufanyiwa marekebisho. “Katika uhakiki wa maombi tumebaini waombaji 2,982 fomu zao zina kasoro. Tumetoa muda wa siku nne, na baada ya hatua hiyo kukamilika tutaan...