Ishu ya mkopo kwa Wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania bado ipo kwenye headlines ambapo leo Jumamosi November 11 2017 Mtandao wa Wanafunzi Tanzania umezungumza kwa dakika zaidi ya 30 kutoa dukuduku lao.
Sisi hatuna ukorofi wala mgogoro na Serikali, bodi wala Wizara na tunatambua jitihada zinazofanywa na Serikali kuitoa elimu yetu sehemu moja kuipeleka kwenye hatua nyingine lakini bado kuna changamoto ambazo tunatakiwa kuzisema.
“Juzi Bungeni Waziri Profesa Ndalichakobaada ya kuulizwa kuhusu mikopo ya elimu ya juu tunamshukuru alijibu kuhusu udahili na usajili vyuoni lakini kuna swala ambalo mpaka anamaliza hakulitolea ufafanuzi wowote, mpaka anamaliza hakuna jibu lolote ambalo lilienda kwa Wanafunzi sisi tuliokosa mkopo hatma yetu ni nini?”
Wanafunzi elfu 31 waliokosa mkopo hatma yao haisemwi, Mkurugenzi tu anaamka inasemekana hawa Wanafunzi wamekosa mikopo kwa kukosa vigezo………….. sio kweli, tatizo sio vigezo…. tatizo ni bajeti iliyotengwa ni ndogo
Tunamuomba Mh. Rais, tunamuomba, tunamuomba Mh. Rais… swala la ada kama mkopo liwe ni swala la lazima, utoaji wa mkopo iwe ni kwa kila Mwanafunzi anaedahiliwa elimu ya juu… laiti Serikali ingelipia ada kila Mwanafunzi alafu ikawabagua kwenye vitu vingine kama pesa ya chakula na malazi tusingelalamika hivi
Bonyeza play hapa chini kutazama kila walichosema Wanachuo hawa..