Uandaaji wa taarifa kwaajili ya tovuti, application, na majukwaa ya mtandani

Masshele Swahili Uchapishaji wa habari mtandaoni kupitia tovuti, app, na majukwaa ya mtandaoni ni miongoni mwa njia maarufu za kutolea habari za kuaminika. Mfano wa tovuti za habari ni Dw kiswahili, BBC Swahili, Cri, Millardayo , fullshangwe, masshele Swahili, mfano wa wa majukwaa ya mtandao yanayotoa habari ni Jamii forum wakati app za habari ni kama vile muungwana app, Millardayo nk Emanuel G, mwandishi wa mtandao kwa muda mrefu anasema kwamba " Uandaaji wa taarifa kwaajili ya kuchapa katika tovuti au majukwaa ya habari unahitaji umakini mkubwa ili kuendana na matakwa ya msomaji, wakati huo huo ukizingatia uandishi wa kiweledi, ambapo mwandishi unapaswa kuandika kwa mtiririko unaoeleweka, kuzingatia taratibu za kiuandishi na kuhakikisha makosa ya kisarufi na kiuakifishaji ya naepukwa huku ukitumia lugha bora" Hivyo katika kutayarisha habari kwaajili ya tovuti huna budi kuzingatia mambo kadhaa Mambo ya kuzingatia Andaa maudhui bora, yenyewe kuzingatia u kweli,...