Masshele Swahili
Uchapishaji wa habari mtandaoni kupitia tovuti, app, na majukwaa ya mtandaoni ni miongoni mwa njia maarufu za kutolea habari za kuaminika. Mfano wa tovuti za habari ni Dw kiswahili, BBC Swahili, Cri, Millardayo , fullshangwe, masshele Swahili, mfano wa wa majukwaa ya mtandao yanayotoa habari ni Jamii forum wakati app za habari ni kama vile muungwana app, Millardayo nk

Emanuel G,  mwandishi wa mtandao kwa muda mrefu anasema kwamba

"Uandaaji wa taarifa kwaajili ya kuchapa katika tovuti au majukwaa ya habari unahitaji umakini mkubwa ili kuendana na matakwa ya msomaji, wakati huo huo ukizingatia uandishi wa kiweledi, ambapo mwandishi unapaswa kuandika kwa mtiririko unaoeleweka, kuzingatia taratibu za kiuandishi na kuhakikisha makosa ya kisarufi na kiuakifishaji ya naepukwa huku ukitumia lugha bora"

Hivyo katika kutayarisha habari kwaajili ya tovuti huna budi kuzingatia mambo kadhaa
Mambo ya kuzingatia

Andaa maudhui bora, yenyewe kuzingatia u kweli, na ushahidi,  tumia lugha faafu, jua wasomaji wako wanahitaji nini na kwa wakati gani, tumia picha zinazoendana na tukio au picha za tukio lenyewe kisha tolea maelezo.  Epuka taarifa za uongo,  Kumbuka kuwa maelezo mengi humchosha msomaji.

hakikisha kichwa hakipotoshi habari, hariri maudhui yako vizuri, kwakuwa wasomaji wa habari wanahitaji uhuru hakikisha kuna nafasi ya kutoka maoni yao, futa maoni ya matusi, epuka kujibu maoni kwa lugha ya matusi.
Katika kipengele hiki kama unachapisha maudhui yaliyokwisha kuchapishwa Tena ni busara kuonesha chanzo.

Baada ya kuchapisha maudhui ya habari

Unaweza kuyatandaza katika mtandao ya kijamii kwa kutumia kiungo Bila kumlazimisha msomaji kusoma kilicho andikwa.