Posts

Showing posts with the label Technology

WhatsApp kuja na mfumo mpya

Image
    Application ya WhatsApp iko kwenye majaribio ya kuweka mfumo mpya wa kusikiliza ujumbe wa sauti (Voice Message/Notes) ambao utawezesha watumiaji kuendelea kusikiliza ujumbe huo hata ukiwa umefunga chat tofauti na ambayo ujumbe huo umetumwa. Mapinduzi haya ya Teknolojia yanakuja kurahisisha watumia wa App hii ambapo awali ilikuwa ukiifungua chat nyingine Voice Message inaacha ku-‘play’ na kukulazimu ubaki katika chat hiyo mpaka mwisho wa kusikiliza ujumbe. Wakati unaundelea kusikiliza juu itatokea mstari wa rangi ambayo inafanana na Audio Player ambayo itaonyesha jina na profile ya aliyekutumia sauti (Voice Message/Notes)

Kwanini unatakiwa kumfuatilia mtoto wako anapokua mtandaoni?

Image
Watoto wanatakiwa kulinda wakati wote wanapoingia mtandaoni. Picha|Mtandao. Ni njia mojawapo ya kumlinda mtoto wa uhalifu wa mtandaoni unaoweza kumpotezea mwelekeo wa maisha. Pia ni kumuepusha na ukatili wa kijinsia unaoweza kukatiza ndoto zake za elimu.  Ni wazi kuwa teknolojia inakua kwa kasi kiasi cha kufanya mifumo ya kujifunza na kufanya mambo kuwavutia watu wengi hasa watoto wenye kudadisi kinachojiri mtandaoni.  Baadhi ya watoto wamekuwa wakitumia simu na kompyuta za wazazi wao kuingia mtandaoni ili kujifunza na kuburudika. Lakini wakati mwingine huwa tofauti kwa sababu baadhi ya mambo yanayopatikana mtandaoni yana madhara kiakili na kiafya kwa mtoto. Hapo ndipo inakuja dhana ya wazazi kuwafuatilia watoto wao wanapokua mtandao ili kujua ni vitu gani wanaangalia na kwa kiasi gani vinachangia kuharibu au kuwakuza katika maadili mema.  Japokuwa bado kuna mjadala katika jamii wa umri sahihi ambao mtoto anatakiwa kuachwa huru bila kuingilia kwa kile...

Microsoft sasa jino kwa jino na Google katika utoaji wa taarifa

Image
Imefanya maboresho ya kitafutishi chake cha Microsoft Edge ili kuwapa wateja wake uwezo mkubwa wa kupata vitu wanavyotafuta mtandaoni. Hatua hiyo inaweza kuleta ushindani mkubwa na kampuni nyingine za teknolojia kama Google inayomiliki kitafutishi cha Chrome. Dar es Salaam. Kampuni ya teknolojia ya Marekani ya Microsoft imefanya maboresho ya kitafutishi chake (Web Browser) kiitwacho  Microsoft Edge  ili kuwaleta karibu watumiaji wa bidhaa zote zinazotumia mfumo wa Microsoft katika kutafuta mambo mbalimbali kwenye mtandao. Kampuni hiyo imeamua kutanua matakwa ya wateja wao na kuwawezesha kupata matokeo mengi zaidi kama ilivyo katika kitafutishi cha Chrome kinachomiliwa na kampuni shindani ya Marekani ya Google. Huenda hatua hiyo ikaleta mashindano makubwa kati ya kampuni hizi mbili baada ya Microsoft kuamka na kuwapa wateja wake kile walichokuwa wanakikosa hapo awali. Maboresho hayo yameenda sambamba na mwonekano mpya wa kitafutishi hicho kwa kubadili nembo yake...

M-PESA MASTERCARD INAVYOWEZA KUBADILI BIASHARA YAKO

Image
-Unaweza kununua bidhaa yeyote mtandaoni ikiwa mahala popote ulimwenguni kwa kupitia M-pesa -Inakupatia card number pamoja na security code utakazo zitumia kufanya malipo mtandaoni -Utaweza kuweka fedha katika kadi yako na kufanya miamala kadiri upendavyo -Ni rahisi kutumia Hujambo ndugu msomaji,  Karibu tuangazie namna muunganiko wa mpesa na MasterCard unavyo weza kuinufaisha biashara yako. Maendeleo ya kiteknolojia ni ahueni katika nyanja zote, na hii sekta ya biashara haijaachwa nyuma katika suala hilo. Kupitia Mpesa master card unaweza kulipia na kutangaza bidhaa yako katika mitandao yenye wafikiaji wengi kama vile Facebook na Instagram hivyo itakuongezea Wateja wengi na wapya kutoka sehemu mbalimbali. Vilevile inakuwezesha kununua bidhaa mbalimbali kutoka maduka ya mtandaoni  ambayo yanapokea malipo ya MasterCard. Sio hivyo tu bali unaweza kupokea malipo ya bidhaa zako kupitia program hii rahisi. Licha ya hayo program hii ni rahisi sana kutumia, kama ili...

Facebook yajipanga kuunda bodi huru kusimamia maudhui

Image
Facebook yajipanga kujiweka kando kusimamia maudhui ya watumiaji wake. Picha|Mtandao. Bodi hiyo itakuwa na wataalam mbalimbali kwa ajili ya kufuatilia maamuzi ya uhariri wa maudhui ya mtandao huo. Huenda itasaidia kupatikana kwa haki za watumiaji kutokana na kesi mbalimbali zinazohusu maudhui. Huenda watumiaji wa mtandao wa Facebook wakapata haki katika maamuzi ya kesi zinazohusiana na maudhui ya mtandao huo baada ya kuwepo kwa mipango ya kuundwa kwa bodi huru itakayokuwa inafuatilia uhariri wa maudhui ya mtandao huo.  Mpango huo unakuja wakati Facebook ikikabiliwa na shutuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya taarifa za watumiaji wake lakini kuwepo kwa maudhui yanayohamasisha chuki na uhasama katika jamii.  Mtandao huo, ulioanzishwa na kuongozwa na raia wa Marekani, Mark Zuckerberg utatumia miezi sita kuunda bodi hiyo ambayo inaweza kutoa mfumo mpya kwa ajili ya kufungua kanuni na njia mpya kwa watumiaji kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya uhariri. Bodi h...

Facebook kuingiza sokoni pesa mpya ya kidigitali

Image
Mtandao wa kijamii wa Facebook umetangaza kuingiza sokoni pesa mpya ya kidigitali sokoni. Tangazo hilo kutoka Facebook linasema pesa hiyo mpya ya kidigitali itayoingizwa sokoni mwaka 2020 itaitwa “Libra”.Pesa hio pia itakubalika katika mifumo ya malipo kama vile Visa na Mastercard. Taarifa hiyo inasema baada ya kuingizwa sokoni pesa hiyo ya kidigitali itaanzishwa pia pochi ya kidigitali ya kuhifazia pesa hio iitwayo “Calibra”. Taarifa hiyo inasema huduma hiyo kwa watumiaji itawezesha kuokoa pesa pia matumizi na kutumiana pesa miongoni mwao. Katika taarifa hiyo ya Facebook imekumbushia kwamba pesa hiyo ya kidigitali na pochi ya kidigitali vitaweza kutumiwa katika na mtu yeyote ambaye kwenye simu yake ana program tumizi za  Facebook Messenger, WhatsApp au “Calibra”.

Unayotakiwa kuyafanya kuimarisha huduma kwa wateja mtandaoni

Image
Jibu kwa wakati meseji za wateja kwa upole na hekima huku ukilenga kutoa jawabu kwa kila swali unaloulizwa. Wape nafasi ya kutoa maoni na mrejesho wa matumizi ya bidhaa na huduma yako. Ni dhahiri kuwa biashara nyingi kwa sasa ziko mtandaoni na kwa sehemu kubwa mitandao ya kijamii inatumika kama jukwaa muhimu la kuwafikia wateja na kukidhi mahitaji yao.  Kama ilivyo mikakati mingine ya masoko, wateja waliopo mtandaoni nao wanahitaji huduma kwa mteja. Wanatakiwa kusikilizwa na kutatuliwa changamoto zao kwa wakati ili kujenga imani na uaminifu katika bidhaa na huduma zako.  Kama bado hujui ufanye nini kuimarisha kitengo cha huduma kwa mteja mtandaoni? Basi fanya mambo haya yanayoweza kukusaidia kutoa huduma nzuri mteja mtandaoni: Uwe msikivu, mwenye hekima na msaidizi Mfanyabiashara kila unapokutana na wateja mtandaoni, jitahidi uwe msikivu, mtulivu, mwenye hekima na msaidizi kwa wateja wako kwa kila swali au ufafanuzi watakaoutaka kutoka kwako.  Epuka ...

Gmail kuja na mabadiliko makubwa mwanzoni mwa Julai 2019

Katika maboresho hayo, kutakuwa na huduma ya kukubali au kukataa wito kwenye tukio, kujaza maswali, kujibu maoni, na orodha za kuvinjari(browsing catalogs). Maoni ya kwenye Google Docs sasa yatakuja  moja kwa moja kwenye barua pepe ya mtumiaji ili aweze kujibu maoni hayo kwa haraka. Dar es Salaam . Mwanzoni mwa mwezi ujao huduma ya barua pepe ya Google (gmail) itafanyiwa maboresho kwa kuongezewa kipengele  kinachoitwa 'dynamic email'  ikiwa ni moja ya mabadiliko makubwa ambayo Google imeyafanya baada ya yale ya mwaka jana ya kalenda na sehemu ya notebook (task bar) ambayo yalimfanya mtumiaji asiishie kutuma na kupokea baruapepe tu. Mabadiliko hayo makubwa kwenye gmail, ambayo yalianza kupatikana kwa majaribio (beta version) tangu Machi mwaka huu kwa wateja wa biashara, sasa yataanza kutumika rasmi kuanzia Julai 2. Katika maboresho hayo, mtumiaji wa barua pepe ataweza kuifanya isibadilike kwenye akaunti zake zote  (default on all Gmail accounts) huku a...

China imezindua 'Chip' inayoweza kuongea na ubongo wa binadamu

Image
Chip ya "Talker Brain" inaweza kufungua fursa ya kutumika katika  maeneo kama vile matibabu, elimu, maisha ya nyumbani na michezo ya kubahatisha ili kuongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa katika maeneo hayo. Picha|Mtandao. “Chip” hiyo inaweza kusoma taarifa zinazopatikana katika mishipa midogo ya ubongo. ni hatua ya kuboresha ufanisi wa mawasiliano kati ya binadamu na mashine.  Inaweza kutumika katika maeneo kama vile ya matibabu, elimu, maisha ya nyumbani na michezo ya kubahatisha. Dar es Salaam.  Kwa mara ya kwanza China imezindua ‘chip’ ya kompyuta inayoweza kusoma shughuli zinazofanywa na ubongo wa binadamu, ikiwa ni hatua ya kuboresha ufanisi wa mawasiliano kati ya binadamu na mashine.  “Chip” ni kipande kidogo  kinachofanya muunganiko  wa sehemu mbalimbali za Kompyuta ambacho kimeundwa na Saketi mbalimbali ambapo  mara zote kipo kwenye mfumo wa “Silcon”. “Chip” ndiyo imebeba mfumo mzima wa umeme kwenye Kompyuta.  Kwa muj...

Ajira zaidi ya milioni 2 zinawasubiri wasichana wanaosoma masomo ya sayansi

Image
Inakadiria kuwa katika kipindi cha miaka 10 ijayo kutakuwa na ajira zaidi ya milioni 2 za teknolojia ambazo hazitajazwa kwa sababu ya ukosefu wa wataalam wa digitali. Changamoto hiyo inafungua mlango kwa wasichana duniani kufaidika na fursa hiyo kwa kuongeza kasi ya kusoma masomo ya sayansi. Baadhi ya wasichana wa Tanzania wameanza kuchangamkia fursa hizo kwa kubuni mifumo ya utatuzi ya kidijitali. Dar es Salaam.  Huenda wanafunzi wa kike wanaosoma masomo ya sayansi katika shule za sekondari na vyuo vikuu wakaboresha maisha yao, baada ya kubainika kuwepo kwa pengo la wataalam wa dijitali duniani.  Kwa mujibu wa Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) unakadiria kuwa katika kipindi cha miaka 10 ijayo kutakuwa na  ajira zaidi ya 2 milioni za teknolojia  ambazo hazitajazwa kwa sababu ya ukosefu wa wataalam wa digitali. ITU inasema changamoto za ajira zinafungua mlango kwa wasichana duniani kufaidika na fursa hiyo kwa kuongeza kasi ya kusoma masomo ya...

UDSM yatakiwa kuongeza kasi utoaji haki miliki kwa wavumbuzi

Image
Sera ya umiliki wa Mali-Akili ya mwaka 2008 inataka Chuo Kikuu kupata kinga ya kisheria katika kutangaza na kuuza kibiashara bidhaa zinazohusiana na Mali-Akili kadri itakavyokuwa inafaa kwa maslahi ya Chuo, mtafiti na umma kwa jumla. Picha|Mtandao. Hatua hiyo inakuja baada ya CAG kubaini kuwa kuna usimamizi na utangazaji duni wa Mali-Akili chuoni hapo. Tangu mwaka 1981 hadi Januari 2018 Chuo kiliweza kutengeneza mashine 66, lakini uvumbuzi mmoja tu ndiyo ulikuwa na haki miliki. Imeshauriwa kutengeneza mifumo imara ya kuchunguza vumbuzi zinazokidhi kupata haki miliki na kufikiria kutoa motisha kwa wavumbuzi bora. Dar es Salaam.  Wakati watanzania wakiungana na wenzao duniani kuadhimisha Siku ya Mali-Akili Duniani ( World Intellectual Property Day ), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimetakiwa kutengeneza mfumo mzuri wa usimamizi na kuendeleza vumbuzi mbalimbali zenye sifa ya kupata haki miliki.  Siku ya Mali-Akili Duniani huadhimisha Aprili 26 ya kila mwaka...

Facebook App yaja kivingine

Image
Muonekano wa ukurasa wa Facebook App ambao unatoa sababu za kwanini mtumiaji anapokea matangazo kwenye ukurasa wake.Picha|Mtandao. Sasa kuwawezesha watumiaji wake kufahamu kwanini matangaza ya biashara au habari zinawafikia katika kurasa zao. Hayo ni miongoni mwa maboresho yanayofanywa na Facebook ili kuwarahisishia watumiaji wake upatikanaji wa huduma bora zinazokidhi mahitaji yao. Dar es Salaam.  Katika kuhakikisha inasogeza huduma zake karibu na watumiaji, mtandao wa Facebook umefanya maboresho katika programu yake tumishi (Facebook App) ambapo mtumiaji ataweza kupata sababu zinazoeleza kwanini tangazo au habari imewekwa kwenye ukurasa wake.  Hatua hiyo huenda ikatatua changamoto ya watumiaji wa mtandao huo kupata matangazo bila ridhaa yao au bila kujua sababu za tangazo husika kuwekwa kwenye ukurasa. Maboresho hayo yanajikita katika mambo mawili ya "Kwa nini ninaona chapisho hili?"( Why am I seeing this post?) na  "Kwa nini ninaona tangazo hili?...

Kwanini wafanyabiashara wanawekeza katika matumizi ya mitandao ya kijamii?

Image
Ni nafuu na rahisi kuwafikia wateja wengi kwa wakati mmoja na inasaidia kuimarisha mahusiano ya kibiashara bila kuathiri umbali na mazingira ya muuzaji na mtumiaji wa bidhaa au huduma.  Ni njia mojawapo ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia na sayansi yanayotokea duniani katika utendaji wa sekta mbalimbali za uzalishaji na manunuzi. Ni ukweli usiopingika kuwa kutokana na kukua kwa teknolojia, matumizi ya mitandao ya kijamii katika shughuli mbalimbali yamepewa kipaumbele zaidi  kuliko siku za nyuma.  Moja ya matumizi ya mitandao ya kijamii ni katika biashara ambapo wajasiriamali hasa vijana wanaomiliki simu janja hupendelea kutangaza biashara zao katika mitandao hiyo  ili kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi na kwa urahisi zaidi. Kuna sababu kadha wa kadha zinazowafanya wajasiriamali wengi kuwekeza katika kutangaza biashara zao mtandaoni kutokana na tafiti iliyofanywa na mtandao wa  three girls media umebainisha mambo mbalimbali yanayowasukuma wa...

Miaka 15 ya Gmail inavyoongeza thamani bidhaa za Google

Image
Gmail imeendelea kuwa maarufu kwa watumiaji kutokana na maboresho inayofanya kila inapohitajika. Picha|Google. Barua pepe ya Gmail ilianzishwa rami mwaka 2004 ambapo imekuwa nyenzo muhimu ya kuipaisha kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya Google duniani. Gmail ina watumiaji zaidi ya 1 bilioni na haina dalili ya kushuka chini. Imekuwa mshindani mkubwa wa barua pepe zingine za Yahoo, Hotmail, Zoho na GMX. Kama wewe ni mtumiaji wa bidhaa za Google hasa barua pepe ya Gmail huenda utakuwa umegundua kitu tofauti katika matumizi yako tangu Aprili 1, 2019.  Kila ukifungua mtandao huo utakutana na neno ‘ Gmail turns 15 ’ likiwa na maana kuwa Gmail inaadhimisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004.  Gmail ambayo imejipatia umaarufu mkubwa duniani, imeendelea kuwa nyenzo muhimu ya kutuma na kupokea barua pepe zinazotumika kwa shughuli mbalimbali za ofisi, biashara na mambo binafsi.  Barua pepe hiyo ambayo inahudumia zaidi ya  watumiaji 1 bilioni ...