MAAJABU YA PENSELI USIYO YAJUA KUHUSU KALAMU HII YA RISASI

Naomba Penseli NA MWANDISHI WETU NCHINI UINGEREZA HAIGHARIMU pesa nyingi, inaanza kufanya kazi mara moja, na haina uzito mkubwa. Inaweza kuwekwa mfukoni vizuri. Haitumii umeme, haivuji, na alama zake zinaweza kufutwa. Watoto huitumia wanapojifunza kuandika, wachoraji huitumia kuchora picha za kupendeza, na wengi wetu huitumia kuandika habari fupi-fupi. Naam, kifaa hicho chenye bei rahisi na kinachotumiwa sana ulimwenguni ni penseli. Penseli ilivumbuliwa bila kutarajiwa katika maeneo ya vijijini huko Uingereza. Acheni tuwasimulie jinsi ilivyogunduliwa na kutengenezwa. Risasi Nyeusi Katika karne ya 16, mabonge ya kitu fulani cheusi yaligunduliwa chini ya kilima cha Borrowdale, kwenye bonde la Wilaya ya Lake kaskazini mwa Uingereza. Ingawa madini hayo yalifanana na makaa ya mawe, hayangeweza kuungua; nayo yaliacha alama nyeusi inayong’aa iliyoweza kufutwa. Kwa kuwa kitu hicho kingebaki kwenye vidole mtu alipokigusa, watu walifunika mabonge ya kitu hicho kwa ngozi y...