Posts

Showing posts with the label dkt mahenge

UANDISHI

  SURA YA KWANZA UANDISHI 1.0 Uandishi maana yake nini? Uandishi ni uwakilishaji wa lugha kwa njia ya maandishi kwa kutumia ishara na alama - yaani mfumo wa uandishi wa lugha husika. Lugha kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu ni “mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa taifa au kundi fulani kwa ajili ya kuwasiliana” (KKS: 201). Tafsiri ya lugha na ile ya uandishi zikiwekwa pamoja, tunaweza kufafanua kuwa, uandishi ni njia ya mawasiliano ambayo wanajamii hutumia lugha ili kuwasilisha mawazo yao kwa njia ya maandishi. Maandishi yanalenga kumpata msomaji atakayesoma kile kilichoandikwa na mwandishi; na kinyume chake kuna masimulizi ambayo yanalenga kumpata msikilizaji. Kwa hiyo, tuna msomaji kwa upande mmoja na msikilizaji kwa upande wa pili. Yote hayo yanawezeshwa na uwepo wa lugha. Uandishi upo wa aina mbalimbali kama vile: uandishi wa habari, uandishi wa kiweledi, uandishi wa kitaaluma, na uandishi wa kub...