UONGOZAJI NA UTOAJI WA HABARI MITANDAO YA KIJAMII

Masshele Swahili. Mitandao ya kijamii ni sehemu mojawapo ya kutolea habari za uhakika, ambapo huwaza kuenea kwa haraka zaidi. Karibu vituo vyote vya redio na televisheni vinazo kurasa maalumu za kutolea habari katika mitandao ya kijamii, kwa mfano katika mtandao wa kijamii wa facebook utakutana na kurasa kama vile, Azamtv, EATV, ITV TANZANIA, MASHELE KISWAHILI, CITIZEN RADIO KBC TBC, na kadhalika. Kurasa hizi ni muhimu katika utoleaji wa habari, na mara nyingi huripoti matukio ya yanayotokea kwa muda huo (breaking news) Jinsi ya kuandaa habari katika mtandao ya kijamii Kwanza nilazima ziwe za u kweli, unapaswa kuepuka utumizi wa maneno mengi( andika kwa ufupi na inayoeleweka) picha mahususi ni muhimu ili kurahisisha uelewekaji wa tukio, tumia lugha ya staha, epuka kuwajibu vibaya wasomaji maana Mara nyingine huweza kukuudhi, futa comment za matusi kama muda unakuruhusu, Chonde chonde hariri taarifa kabla ya kuiweka kwa umma. Sikiliza wateja wako, ta...