Masshele Swahili.
Mitandao ya kijamii ni sehemu mojawapo ya kutolea habari za uhakika, ambapo huwaza kuenea kwa haraka zaidi. Karibu vituo vyote vya redio na televisheni vinazo kurasa maalumu za kutolea habari katika mitandao ya kijamii, kwa mfano katika mtandao wa kijamii wa facebook utakutana na kurasa kama vile, Azamtv,  EATV, ITV TANZANIA, MASHELE KISWAHILI, CITIZEN RADIO KBC TBC, na kadhalika.
Kurasa hizi ni muhimu katika utoleaji wa habari, na mara nyingi huripoti matukio ya yanayotokea kwa muda huo (breaking news)

Jinsi ya kuandaa habari katika mtandao  ya kijamii
Kwanza nilazima ziwe za u kweli, unapaswa kuepuka utumizi wa maneno mengi( andika kwa ufupi na inayoeleweka)  picha mahususi ni muhimu ili kurahisisha uelewekaji wa tukio, tumia lugha ya staha, epuka kuwajibu vibaya wasomaji maana Mara nyingine huweza kukuudhi, futa comment za matusi kama muda unakuruhusu, Chonde chonde hariri taarifa kabla ya kuiweka kwa umma.
Sikiliza wateja wako, tafuta wakati gani wanajishughulisha na mtandao na ulenge taarifa zako kwa majukwaa tofauti.
Maingiliano na wateja yanahitaji pande mbili. Watangazaji wanatakiwa kujibu maswali na matamshi muafaka mtandaoni, ama sivyo wateja wanaweza kuona wanatengwa.
“Daima kumbuka kutafuta njia mpya ya kuwasiliana na wateja wako” – Leyla Najafli – mtayarishi wa  taarifa za mitandao ya jamii, BBC World Service.
Baadhi ya mitandao unayoweza kuchapisha habari ni Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat na mitandao mengine ya kijamii yote inatumia mitindo tofauti kwa hivyo ni muhimu kubadilisha video zako, maandishi na picha.
Pia ni muhimu kuibadilisha lugha ya matusi au chuki. Watu wanafaa kuwa na uhuru wa kueleza maoni yao kwenda mtandao, lakini sio ikiwa ataumiza mtu mwengine au kumtia hatarini