kanuni za kifonolojia
Mpaka sasa mjadala umehusu vipashio vya kifonolojia, hususa fonimu na alofoni. Lakini kila mjua-lugha anatambua kuwa watu hawazungumzi kwa kutumia fonimu moja moja. Hata kama tukiweza kuorodhesha fonimu zote za lugha fulani pamoja na alofoni zao, bado tutakuwa hatujajua mfumo wa fonolojia wa lugha hiyo ulivyo. Katika kutumia fbnimu za lugha ili kuunda maneno, na kufanikisha mawasiliano, kuna kanuni za msingi ambazo kila lugha inazifuata. Kanuni ya jumla sana, na ambayo tumekwishaigusia katika kurasa zilizotangulia, ni ile ya mfuatano unaoruhusiwa wa fbnimu za lugha fulani; na katika kanuni hii, lugha hutofautiana sana. Katika lugha ya Kiingereza, kwa mfano, vipasuo sighuna /p, t, k/ vinaweza kufuata kikwamizi /s/ lakini vipasuo ghuna /b, d, g/ haviwezi. Hivyo kuna maneno: 28 {spar, star, scar}, lakini hakuna 29 *{sbar, sdar, sgar} Wazungumzaji wa Kiingereza wanajua wazi kuwa maneno ya (29) hayawezi kuwa maneno ya lugha yao kwa sababu hayaruhusiwi na kanuni za ki...