SIFA MAJUMUI ZA LUGHA KATIKA FONOLOJIA

Katika sehemu iliyopita tumesema kwamba lengo kuu la fonolojia ni kujaribu kuziweka wazi baadhi ya sifa majumui  zinazojitokeza katika lugha asilia. Maelezo hayo yamejengeka kwenye mantiki kwamba pamoja na ukweli kuwa kunatofauti za wazi  zinazojitokeza  klatika fonolojia ya mifumo mbalimbali ya lugha asilia, bado kuna tofauti fulani ambazo zinaelezwa kuchangiwa lugha zote na lugha zote asilia ndizo zijulikanazo katika taaluma ya fonolojia kama SIFA MAJUMUI ZA LUGHA.

 

-          KUNA AINA KUU TATU ZA SIFA MAJUMUI ZA LUGHA.

Ambazo ni sifa majumui halisi za lugha, sifa majumui pana za lugha, na sifa majumui tabirifu za lugha.

 

SIFA MAJUMUI  HALISI ZA  LUGHA-  Ni zile sifa za kiisimu ambazo ni zakawaida katika lugha zopte za kibinadamu . mfano katika lugha zote kuna irabu a’ na nikwaidsa katika lugha zote kuwa na utaratibu wa konsonanti na irabu ingawa hutofautiana katika idadi baina ya lugha moja na nyingine

 

SIFA MAJUMUI ZA LUGHA PANA.

Ni zile sifa amabazo hupatikana katika lugha nyingi ingawa sio zote. Mfano wanaisimu wengi hukubaliana kuwa kila lugha ina angalau irabu tano, lakini ukweli nikuwa kuna baadhi yalugha zina irabu tatu tuu

 

SIFA MAJUMUI TABIRIFU, Wataalamu wamegundua kuwa kuna mazingira flani flani katika lugha ambapo kutokea kwa sauti flani huashiria kutokea kwa sauti nyingine flani, kuwepo kwa sifa flani ya msingi basio huashiria kutokea kwa sifa nyingine