Posts

Showing posts with the label Michezo

USAJILI SIMBA :SIMBA NIKAMA WAMESHINDWA KWA ASANTE KWASI YAJULIKANA ANAMKATABA NALIPULI

Image
Simba inaonekana kama imekwama kumsajili beki Asante Kwasi. Taarifa zinasema, Simba imegundua Kwasi ana mkataba wa miezi saba na Lipuli ya Iringa, jambo ambalo limewakatisha tamaa. Simba ilikuwa imemficha Kwasi jijini Dar es Salaam kusubiri kumalizana naye baada ya wakala wake kusema hakuwa na mkataba na Lipuli. Lakini baada ya kufanya uchunguzi wa kina kupitia kamati yake ya usajili, iliamua kufunga breki ili kutafakari kwanza kuangalia kama inawezekana kujadiliana na Lipuli au kuachana naye. Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufungwa saa sita na dakika moja, na inaonekana umebaki muda mchache Simba kumaliza na Lipuli ingawa ilielezwa kuna juhudi zilikuwa zinafanywa. KUJIUNGA NA KAMPUNI ZA KUBETI Pmbet tanzania app  jisajili  na upakue >> HAPA >> Betway tanzania app  jisajili na upakue >> HAPA >> Gal sport  jisasajili na upakue kwakubofya >>  HAPA >>

SIMBA MPYA : HIKI NDICHO KIKOSI CHA SIMBA , WAPINZANI WAJIPANGE KISAIKOLOJIA

Image
Baada ya simba  kufanya usajili Wa wachezaji watatu wakigeni  Huenda kikosi cha miamba hiyo ya Tanzania kikafanyiwa marekebisho kiasi na hiki ndicho kikosi kinachotarajiwa kuanza ambapo itazibidi timu pinzani kujipanga kisaikolojia kulingana na Amina ya wachezaji waliopo simba kwani hakuna mchezaji mwenye afadhali katika kikosi hicho KIKOSI CHA SIMBA KINAWEZA KUWA HIVI 1:manula 2:nyoni 3:zimbwe jr 4:kwasi 5-kotei 6:mkude 7:shiza 8niyonzima 9:domingos 10:okwi 11:mo ibrahim SUB mseja,ally shomar,mwambeleko,mzamiru,boko,sakuwaha,juuko,mlipili,luizio,bukaba KUJIUNGA NA PARMACH TZ NA KUPAKUA  PARMACH APK   BOFYA >>> HAPA >>> kisha jaza taarifa zako udeposit kupokea bonasi 22bet tanzania  app  jisajili na upakue kwa kubofya >> HAPA >> Pmbet tanzania app  jisajili  na upakue >> HAPA >> Winprincess   tanzania App  jisajili na upakue >> HAPA >> Betway tanzania app ...

USAJILI VPL:GYAN, MAVUGO WALIVYOTEMWA MAJEMBE MATATU YALIYOTUA SIMBA, USAJILI JANGWANI, AZAM, SINGIDA, ALIKOKWENDA NGASSA NA USAJILI WOTE KWAUJUMLA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR SIMBA SC imesajili wachezaji watatu wapya wa kigeni, beki Mghana Asante Kwasi, kiungo mshambuliaji Mzambia Jonas Sakuwaha na mshambuliaji Antonio Dayo Domingues kutoka Msumbiji. Wakati dirisha dogo la usajililinakaribia kufungwa jana, viongozi wa Simba walikuwa wanahaha kukamilisha usajili huo, hususan wa mchezaji Kwasi, ambaye bado ana mkataba na klabu yake ya sasa, Lipuli ya Iringa. Lakini kwa Sakuwaha na Domingues hakukuwa na tatizo na habari zinasema wachezaji hao watachukua nafasi za beki Mzimbabwe, Method Mwanjali na washambuliaji, Mghana Nicholas Gyan na Mrundi Laudit Mavugo.   Beki Mghana Asante Kwasi (kulia) akiwa na mshambuliaji Antonio Dayo Domingues kutoka Msumbiji Wapinzani wao, Yanga wamesajili wachezaji wawili tu wapya, beki Fiston 'Festo' Kayembe Kanku kutoka Balende FC ya kwao, DRC na mshambuliaji kinda, Yohanna Nkomola ambaye ni mchezaji huru, aliyekuwamo kwenye kikosi cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serenget...

Yondani, Chirwa kamili kuivaa Azam

Image
  Yanga wao wameamua kufanya mambo yao kimyakimya wakijiandaa na mechi ya Jumamosi. Sasa hawana wanachoweza kulaumu maana mechi yao dhidi ya Azam FC itachezwa saa 10 jioni, Jumamosi. Wanachotaka ni kushinda na Kocha Mkuu, George Lwandamina aliagiza mazoezi makali yafanyike na juzi wachezaji walikuwa hoi. Sasa wamelegeza ukali wa mazoezi na wanaendelea na mazoezi ya mbinu zaidi kuhakikisha ushindi unapatikana Jumamosi. Pamoja na kwamba watamkosa Pius Buswita ambaye ana kadi tatu za njano, mshambuliaji Obrey Chirwa kamaliza adhabu yake anarejea. Lakini Yanga watakuwa na uhakika kwamba ukuta utaimarika tena wakati Kelvin Yondani anarejea pia. Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu kubwa, Yanga wakitaka kupunguza pengo lao kubwa dhidi ya Simba na Azam pia lakini Azam FC wakitaka kushinda wazidi kuipa presha Simba iliyo kileleni mwa msimamo.

Azam waapa kuitungua Tanzania Prisons

Image
Kocha msaidizi wa Timu ya Azam Idd Seleman Cheche amesema kuwa wapo tayari kuwavaa 'wajelajela' Tanzania Prisons watakapokutana nao katika mchezo wa ligi utakaofanyika Jumapili ya tarehe 21 Januari, 2018 kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Akizungumza na mtandao wa Azam Fc Cheche amesema kuwa wamerekebisha makosa madogo waliyoyafanya dhidi ya Timu ya Majimaji na kuwa wanatarajia ushindi.  "Plan yetu Jumapili ni kuhakikisha tunapambana kadri ya uwezo wetu ili kupata matokeo, tumeangalia kitu gani kilitukwanza tukijumuisha na uchovu na tutaangalia jinsi ya kurekebisha ili tusirudie makosa", amesema Cheche. Cheche amewataja Tanzania Prisons kuwa timu nzuri ambayo watahitaji umakini mkubwa ili kuwashinda. Timu nzuri "Tanzania Prisons ni wazuri wanapambana lakini tutatumia udhaifu wao ili tuwaangamize na tuhakikishe tunapata alamu tatu muhimu", ameongeza Cheche. Mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi mwaka 2018, tayari wapo Jijini Mbeya ambapo wanaen...

Kocha Mpya wa Simba apagawishwa na Okwi

Image
KIKOSI cha Simba,  Alhamisi kilijitanua kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mchezo huo ambao Simba ilikuwa ikihitaji zaidi matokeo ya ushindi ili ijihakikishie nafasi yake ya kukaa kileleni, ilifanikiwa kupata bao la mapema dakika ya tatu lililofungwa na Shiza Kichuya. Beki wa kati wa timu hiyo, Asante Kwasi, aliongeza bao la pili dakika ya 24 baada ya kukwepa mtego wa kuotea aliowekewa na mabeki wa Singida United. Mara baada ya Kwasi kufunga bao hilo, kocha mpya wa Simba, Pierre Lechantre raia wa Ufaransa, alinyanyuka kwenye kiti chake akiwa jukwaani na kuanza kushangilia pamoja na ofisa habari wa timu hiyo, Haji Manara huku akiwapungia mkono mashabiki wa timu hiyo. Dakika ya 65 wakati Emmanuel Okwi wa Simba anajiandaa kuingia kuchukua nafasi Mzamiru Yasin, mashabiki wa timu hiyo walikuwa wakimshangilia kwa nguvu ...

BREAKING NEWS: HANS POPPE AMPA GARI SAID NDEMLA

Image
Mwenyekiti wa Kamtai ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametoa zawadi ya gari kwa mchezaji wa Simba, Said Hamis Ndemla. Hans Poppe ametangza kumpa Ndemla gari baada ya kuonyesha kiwango kizuri cha kuvutia katika mechi dhidi ya Singida United, leo. Simba imeshinda kwa mabao 4-0 katika mechi hiyo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini. Ndemla alitengeneza mabao mawili moja akifunga Emmanuel Okwi na jingine Asante Kwasi. Hans Poppe amesema mechi ya leo imekuwa ni fainali ya uamuzi wake lakini amekuwa akimfuatilia Ndemla. “Nilikuwa nikimfuatilia kama ambavyo nimekuwa nikisema nahitaji mchezaji mwenye nidhamu na ambaye hawezi kubadilika. Utaona Ndemla amekuwa benchi lakini akiingia uwanjani anaonyesha mchango wake,” alisema. “Tena pamoja na kukaa benchi, hakuwahi kuonyesha utovu wa nidhamu. Badala yake kila akipata nafasi amekuwa akijituma na kuisaidia timu.” Hii ni mara ya pili Hans Poppe anatoa gari kwa mchezaji wa Simba. Alianza n...

Kamati ya saa 72, Mchezaji yanga apigwa stop, waamuzi wapigwa rungu

Image
  Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Saa 72) iliyokutana Januari 4, 2018 imejadili mechi mbalimbali za Ligi Kuu (VPL) Daraja la Kwanza (FDL) na Daraja la Pili (SDL). Ligi Kuu. Mechi namba 72 (Mbeya City 0 vs Simba 1). Kamishna wa mechi hiyo Billy Mwilima amepewa Onyo Kali kwa kuruhusu mchezaji Hamisi Msabila wa Mbeya City kucheza mechi bila kuonyesha leseni, hivyo kukiuka Kanuni ya 14(16 na 17) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Mechi namba 81 (Ndanda 1 vs Njombe Mji 1). Klabu ya Ndanda imepigwa faini ya shilingi 500,000 (laki tano) kwa kutowasilisha orodha ya wachezaji wake (team match list) kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre- match meeting) kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 14(2k) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi ya Ndanda katika mechi hiyo iliyofanyika Novemba 24, 2017 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu. Pia Kamati imeiomba Sekretarieti ya Bodi ya Ligi kutoa W...

Hii ni droo 32 Bora ya Kombe la Shirikisho la Azam Saports

Image
  Ile droo ya 32 Bora za mashindano ya Azam Sports Federation Cup imefanyika leo Ijumaa, Januari 5, 2017 ambapo makundi hayo yamepangwa. Timu 32 zilizofuzu kwenye raundi ya 32 bora ni: Ruvu Shooting, Mwadui FC, Dodoma FC, KMC, Tanzania Prisons, Yanga, Green Worriors, JKT Oljoro, Buseresere FC, Friends Rangers, Majimaji Rangers, Singida United, Pamba SC, Azam FC, Kiluvya FC, Mwadui FC, Mbao FC, Toto Africans. Droo ya Kombe la  FA KMC VS Toto Africans Majimaji Vs Ruvu Shooting Njombe Mji vs Rhino Rangers Kiluvya United   vs  JKT Oljoro Ndanda Vs Biashara United Pamba Vs Stand United Polisi Tanzania Vs Friends Rangers JKT Tanzania Vs  Polisi Dar Ihefu Vs Yanga Mwadui Vs Dodoma Green Warriors Vs  Singida United Burkina FC Vs Tanzania Prison Kariakoo Lindi Vs Mbao Majimaji Rangers Mtibwa Sugar Kagera Sugar Vs Buseresere Shupavu Vs Azam Mechi zitachezwa Januari 31 na Februari Mosi mwaka huu.

Mapinduzi Cup: United yawa timu ya kwanza kufuzu nusu fainali

Image
Timu ya soka ya Singida United imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya mapinduzi Cup inayoendelea huko Unguja Visiwani Zanzibar, baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mlandege FC. Singida United ambao sasa wanafikisha alama 9 baada ya kushinda michezo yote mitatu waliyocheza hadi hivi, wamefunga mabao yao matatu kupitia kwa Danny Usengimana ambaye amefunga kwa njia ya penati katika dakika ya 29. Ilikuwa kama haitoshi Singida United ambao walikuwa wakicheza soka la kushambulia muda wote walipata bao la pili katika dakika ya 37 kupitia shuti kali la guu la kulia la kiungo wa kati Kenny Ally Mwambungu. Bao la tatu la Singida United ambalo lilikamilisha ndoto yao ya kucheza nusu fainali limefungwa na Lubinda Mundia Mbia katika dakika ya 56 baada ya kufanya jitihada binafsi kuuwahi mpira ambao wengi walidhani kuwa mpira ulikuwa unaenda kutoka na kuuzamisha wavuni. Bado mechi mbili. Singida United wanafuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo in...

Mapinduzi Cup 2018: Simba kuwavaa Jamuhuri nao Yanga JKU

Image
Michuano ya Kombe la Mapinduzi itaendelea Alhamisi ya Januari 04 2018 kwa michezo mitatu kufanyika kwenye uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar ambapo Simba na Yanga watajitosa uwanjani.  Mchezo wa kwanza utakuwa wa kiporo kati ya Taifa Jang'ombe dhidi ya Singida United mchezo ambao utafanyika saa 8.30.  Aidha mchezo huo ambao ulilazimika kuhairishwa Baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kufuatia mvua kubwa  ilionyesha na kusababisha uwanja wa Amaan kujaa maji ambapo Singida United walikuwa wakiongoza mchezo huo kwa mabao 3-0.  Saa 10.30 jioni itakuwa zamu ya Mabingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bars Yanga SC dhidi ya wapinzani wao JKU ya kutoka Visiwani Zanzibar huku Sumba SC wakikabiliana na timu ya Jamuhuri katika mchezo ambaoao utafanyika saa 2.15 usiku. Katika mchezo mwingine uliofanyika Jumatano ni URA ya Uganda waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mwenge Fc.

Kocha wa Taifa Stars aipa ubingwa wa VPL Azam

Image
Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania Dokta Mshindo Msolwa, ameitabiria Timu ya Azam kuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu huu . Akizungumza na kipindi cha michezo cha EFM, Msola amesema hayo ni kutokana na klabu hiyo kuwaandalia mazingira mazuri wachezaji wake ndani na nje ya uwanja. -Azam wana huduma zote facilities, mishahara, mazingira kila kitu kizuri", amesema Msolwa. Kuhusu uwezo wa Azam kutwaa ubingwa wa ligi ya Vodacom, Msolwa amesema amebaini kuwa Timu hiyo ina msingi thabiti baada ya kuamua kuwekeza kwenye soka la vijana pamoja na kuwapa nafasi. Msingi dhabiti -Nilijua Azam watafanya vizuri walipofanya mabadiliko ya kutumia vijana na kuacha mazoea ya kusajili majina makubwa tena vijana wasiokuwa na majina", amesema Msolwa. Kadhalika Msolwa amesema kuwa hatua hiyo imeiwezesha timu hiyo kufanya vizuri kwa kuwa vijana hao wana umoja wanapocheza tofauti na wachezaji walio na majina makubwa ambao hucheza kwa masla...

Shomari Kapombe kurudi uwanjani, baada ya miezi mitano

Image
  Mlinzi wa pembeni wa klabu ya Simba Sports Club Shomari Kapombe amesafiri na timu kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Mapinduzi Cup. Kapombe ambaye alisajiliwa na timu hiyo akitokea Azam ameshindwa kucheza mchezo wowote hadi hivi sasa kutokana na kuwa na majeraha aliyoyapata wakati akiitumikia timu ya Taifa dhidi ya Rwanda Julai mwaka uliopita. Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Simba Haji Sunday Manara amesema Kapombe ataanza kuonekana kwenye michuano hiyo pamoja na wachezaji Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi ambao nao walikuwa na majeraha. -Wachezaji Salim Mbonde na Said Mohammed 'Nduda' wao tumewaacha Dar, Ila Kapombe tutajiunga naye Zanzibar ameshaanza mazoezi mepesi mepesi kwa hiyo tutakuwa naye, na Okwi yeye ameshatua nchini na tutakuwa naye," Manara amesema. Simba wamesafiri asubuhi hii kuelekea visiwani Zanzibar ambapo katika michuano hiyo wataanza kwa mchezo dhidi ya timu ya Mwenge FC Jumanne ya Januari 2, 2018. P...

Kikosi cha Simba Vs Ndanda, Djuma afanya mabadiliko makubwa

Image
Kocha Mrundi Masoud Djuma amefanya mabadiliko makubwa katika kikosi cha Simba SC ambacho kitacheza na Ndanda FC katika muendelezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara. Katika mabadiliko hayo Kocha Djuma amewaanzisha kiungo Mohamed Ibrahim 'MO' pamoja na kinda Paul Bukaba ambaye atacheza katika nafasi ya ulinzi. Aidha Pacha wawili Jonas Mkude pamoja na James Kotei kwa pamoja wameanza huku safu ya ushambuliaji ikipambwa na mkongwe John Bocco pamoja na Juma Luizio. Wanaoanza:  Aishi Manula, Paul Bukaba, Erasto Nyoni, James Kotei, Juuko Murshid, Jonas Mkude , Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, John Bocco, Juma Luizio na Mohamed Ibrahim Akiba : Emanuel Mseja, Hussein Mohamed, Jamal Mwambeleko, Yusuph Mlipili, Said Ndemla, Nicholas Gyan na Moses Kitandu. Mchezo huo unatarajiwa kufanyika katika Dimba la Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.

VPL: Wanankurukumbi watia maguu jijini Mbeya, kuwakabili wanakomakumwanya

Image
Kikosi cha timu ya soka ya Kagera Sugar ‘Wanankurukumbi’ kimewasili jijini Mbeya tayari kabisa kufanya maandalizi mepesi kuelekea mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Wanakomakumwanya Mbeya City. Katibu mkuu wa klabu ya Kagera Sugar Hussein Madaki amesema kikosi hicho kipo katika hali nzuri na kwamba wanatarajia kupata ushindi katika mchezo huo ambao utafanyika Jumatatu ya Januari 1, 2018 kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine. -Timu imewasili jijini Mbeya jioni hii, kuhusu mchezo tumejiandaa vizuri kwani tunaamini kuwa hii ni mechi ngumu lakini ni mechi ambayo tunahitaji pointi tatu, na tutajitahidi kuhakikisha tunapata ushindi,” Madaki ameeleza. Amesema wanaenda kwa kucheza na Mbeya City kwa tahadhari kubwa ukizingatia timu wanayokutana nayo ni timu zoefu kwenye ligi lakini pia ni timu ngumu lakini kwa kuwa lengo lao ni kupata pointi tatu basi watasahau yote hayo na kupambana kwa juhudi. Kagera Sugar wanakwenda kucheza na Mbeya City katika nafasi ya 10 kwa kuk...

VPL :AZAM, STEND HATOKI CHAMAZI

Image
  Raundi ya 12 ya ligi kuu soka Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2017/18 inatarajiwa kuanza Ijumaa ya Disemba 29, ambapo mabingwa mara moja wa taji hilo timu ya soka ya Azam FC watawakaribisha Stand United, katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam. Kuelekea mchezo huo ambao unatarajiwa kuanza majira ya saa 1:00 jioni, taarifa kutoka katika klabu ya Azam imesema kuwa wachezaji wote wapo vizuri isipokuwa mchezaji mmoja pekee Mbaraka Yusuph hivyo ni imani yao kuwa mwalimu atakuwa na uwanda mpana wa kupanga kikosi chache. Akitoa taarifa hiyo Jaffary Idd Maganga ambaye ndiye msemaji wa klabu ya Azam amesema hawatawachukulia poa Stand United na wanachotaka wao ni kuingia kwenye mchezo huo na kupata ushindi ukizingatia mchezo wa mwisho wa ligi walitoka sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar. -Ni mchezo mgumu na mchezo ambao unatumia akili nyingi ili kuweza kupata matokeo, niseme tu Mwalimu amepata muda mrefu wa kuiandaa timu, tupo tayari tupo vizuri, majeruhi ni Mba...

BAD NEWS: YANGA KUWAKOSA WACHEZAJI MUHIMU WATANO MECHI YAMBAO

Image
Mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu soka Tanzania Bara, Dar Young Africans watawakosa wachezaji wao muhimu katika mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC ‘Wabishi’, utakaofanyika Jumapili ya Disemba 31 kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza. Wachezaji hao ni majeruhi Donald Ngoma, Thaban Kamusoko na Kelvin Patrick Yondani pamoja na Ibrahim Ajib Migomba ambaye yeye ataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano wakati Obrey Chirwa yeye akiwa bado hajarudi kutoka Zambia alipokwenda kwa ruhusa ya klabu. Dismas Tena ambaye ni mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha klabu hiyo kongwe nchini, amesema kwa kuwa wanawachezaji wengi tayari mwalimu ameshatafuta wachezaji ambao wataziba pengo hilo. -Tayari benchi la ufundi limeshaandaa kikosi kingine ambacho kitaziba mapengo hayo, timu yetu inawachezaji 29 ambao wamesajiliwa , kwa hiyo unaweza kuona kila mchezaji ana umuhimu ni benchi la ufundi tu kuamua nani na nani wa kuwatumia,” alisema Dismas. Mbao ni timu ngumu. Akiw...

BAD NEWS: SIMBA KUWAKOSA WACHEZAJI HAWA MECHI YA NDANDA

Image
Wachezaji wa timu ya Simba. KOCHA wa Simba, Masoud Djuma amesema kuwa kutokana na mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi raia wa Uganda kutokuwa sawa, amelazimika kumpatia mazoezi ya peke yake ili kumuweka fiti huku akitarajiwa kukosa mechi dhidi ya Ndanda mchezo ambao pia ataukosa Haruna Niyonzima. Haruna Niyonzima. Okwi alipatwa na majeraha ya enka hivi karibuni katika mechi dhidi ya Mbeya City ambapo bado anaendelea na matibabu. Akizungumza na Championi Jumatano, Masoud alisema kuwa, Okwi bado hayupo fiti hivyo amemua kumpatia programu maalumu ya kumweka fiti kutokana na majeraha yake ili aweze kurejea katika kiwango chake. “Okwi bado hayupo fiti na hajaanza mazoezi pamoja na wenzie kwa sasa kuna mazoezi nimempatia ambayo anayafanya peke yake ya kuzunguka uwanja pamoja na viungo huku akiendelea kuwa karibu na dokta kwa lengo la kuangalia afya yake. “Siwezi kumtumia mchezaji akiwa bado hajapona vyema kwani nitaweza kumuongezea majeraha zaidi na kuharibu uwezo wake, hivy...

Mchezaji Simba amkingia kifua Joseph Marius Omog

Image
Kocha mzoefu na ambaye aliwahi kuichezea timu ya soka ya Simba Sports Club Madaraka Bendela amesema timu hiyo imefanya haraka kuachana na Kocha Joseph Omog kwani bado alikuwa akihitajika katika timu hiyo. Madaraka ambaye kwa sasa anaishi Jijini Arusha, amesema toka Omog anaingia Simba mwaka jana hadi anaondoka rekodi zake hazikuwa mbaya sana hivyo ilipaswa Simba waendelee kumvumilia na kumpa muda zaidi. -Omog toka anakuja hadi anaondoka amewaacha Simba wakiwa bado wapo nafasi nzuri, amewaacha wakiwa wanaongoza ligi na kama wangeendelea kumuacha na kumpa muda ukizingatia na usajili ambao wameufanya labda angeweza kupata matunda mazuri kwa hapo baadae," amesema. Ushauri kwa makocha.  Madaraka ambaye anasifika kwa kuibua vipaji vingi vya soka nchini kikiwemo cha Erasto Nyoni, ametoa ushauri pia kwa makocha wa mpira kujua sehemu wanayoenda kufanya kazi kabla ya kukubali kazi hiyo. Amesema kila timu inakuwa na falsafa tofauti ya uchezaji mpira hivyo kama mwalimu ukitambua hil...

HE! UMEMSIKIA KOCHAMPYA WASIMBA ?!!?

Image
Kocha aliyekabidhiwa majukumu mazito ya kukinoa kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club, Mrundi Masoud Djuma amesema mipango yake baada ya kupewa kikosi hicho ni kurudisha heshima na morali. Amesema atafanya hivyo kwa wachezaji mashabiki na wanachama wa timu hiyo ambao kwa kuanzia ni lazima aifunge Ndanda FC kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa mjini Mtwara. -Nafahamu mashabiki na wanachama wamepoteza imani na timu yao, lakini nitahakikisha imani yao inarejea na hiyo ni kushinda mechi zijazo, tunachopaswa kukifanya sasa ni kusahau yaliyopita na kuangalia yaliyopo mbele yetu, Bado timu ni nzuri na kikosi ni kipana,” amesema. Djuma alisema katika mazoezi ya Jumapili asubuhi alitumia muda wake kuzungumza na wachezaji ili kila mmoja kujua jukumu lake ndani ya timu, Nataka kila mchezaji aelewe jukumu lake uwanjani, kwani tunachohitaji sasa ni ushindi pekee na si kitu kingine, hivyo Wana Simba wategemee baadhi ya mabadiliko yenye mafanikio katika timu yao,” ali...