Kikosi cha Simba Vs Ndanda, Djuma afanya mabadiliko makubwa



Kocha Mrundi Masoud Djuma amefanya mabadiliko makubwa katika kikosi cha Simba SC ambacho kitacheza na Ndanda FC katika muendelezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.
Katika mabadiliko hayo Kocha Djuma amewaanzisha kiungo Mohamed Ibrahim 'MO' pamoja na kinda Paul Bukaba ambaye atacheza katika nafasi ya ulinzi.
Aidha Pacha wawili Jonas Mkude pamoja na James Kotei kwa pamoja wameanza huku safu ya ushambuliaji ikipambwa na mkongwe John Bocco pamoja na Juma Luizio.
Wanaoanza: Aishi Manula, Paul Bukaba, Erasto Nyoni, James Kotei, Juuko Murshid, Jonas Mkude , Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, John Bocco, Juma Luizio na Mohamed Ibrahim
Akiba: Emanuel Mseja, Hussein Mohamed, Jamal Mwambeleko, Yusuph Mlipili, Said Ndemla, Nicholas Gyan na Moses Kitandu.
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika katika Dimba la Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?