Posts

Showing posts with the label SUA

Taarifa muhimu kwa wanafunzi wa vyuo kutoka Bodi ya Mikopo (HESLB)

Image
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawataarifu wanafunzi wanaonufaika na mikopo kuwa  wanatakiwa kuendelea kuingiza taarifa zao kwa njia ya mtandao kupitia http://olas.heslb.go.tz   hadi tarehe 31 Januari, 2018. Wanafunzi wanufaika wanapaswa kufanya yafuatayo: •    Tembelea mtandao wa http://olas.heslb.go.tz •  Fungua kiunganishi cha “Click here to start” kwenye maelezo ya mwanzo ya kukaribisha. •    Weka namba yako ya mtihani ya Kidato cha Nne na mwaka uliofanya mtihani huo, kwa mfano: S0129.0004.2020 •   Weka namba yako ya akaunti ya Benki kama ilivyowasilishwa HESLB au kama inavyoonekana kwenye “signing sheet” •    Ingiza neno jipya la siri na ulithibitishe. •   Baada ya kuthibitisha, ukurasa wa kuweka picha yako “passport size photo” utafunguka. •    Weka picha yako ya rangi katika ukubwa wa 120×150 •    Wanufaika wapya wa mikopo kwa mwaka wa masomo 201...

MWANAFUNZI SUA ASAKWA KWA KOSA LA KUMNYONGA MPENZI WAKE

Image
 Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamsaka mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Mwita Marwa (30) kwa tuhuma za kumuua kwa kumnyonga mpenzi wake Kibua Adam (39) baada ya kutokea kutokuelewana kati yao. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema tukio hilo lilitokea Januari 22 mwaka huu katika eneo la Modeco Manispaa ya Morogoro ambapo mwanafunzi huyo alitoweka baada ya tukio hilo. Amesema siku ya tukio mwanafunzi huyo na mpenzi wake ambaye ni mhudumu wa baa walichukua chumba katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kama Aluta ambapo walilala lakini baadaye mwili wa marehemu ulikutwa chumbani. “Dada huyu mkazi wa Kihonda alikutwa ameachwa chumbani akiwa ameshafariki na baada ya uchunguzi ilionekana kwamba marehemu alinyongwa shingo kabla ya kifo chake,” amesema Kamanda Matei. Hata hivyo, kamanda huyo amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alimwandikia ujumbe wa simu dada wa marehemu aitwaye Happiness Adamu ujumbe akis...