Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawataarifu wanafunzi wanaonufaika na mikopo kuwa  wanatakiwa kuendelea kuingiza taarifa zao kwa njia ya mtandao kupitia http://olas.heslb.go.tz  hadi tarehe 31 Januari, 2018.

Wanafunzi wanufaika wanapaswa kufanya yafuatayo:
•    Tembelea mtandao wa http://olas.heslb.go.tz
•  Fungua kiunganishi cha “Click here to start” kwenye maelezo ya mwanzo ya kukaribisha.
•    Weka namba yako ya mtihani ya Kidato cha Nne na mwaka uliofanya mtihani huo, kwa mfano: S0129.0004.2020
•   Weka namba yako ya akaunti ya Benki kama ilivyowasilishwa HESLB au kama inavyoonekana kwenye “signing sheet”
•    Ingiza neno jipya la siri na ulithibitishe.
•   Baada ya kuthibitisha, ukurasa wa kuweka picha yako “passport size photo” utafunguka.
•    Weka picha yako ya rangi katika ukubwa wa 120×150
•    Wanufaika wapya wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 hawatahusika kwenye zoezi hili kwa vile taarifa zao ziliwasilishwa wakati wa kuomba mikopo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Tarehe 26/01/2018