Posts

Showing posts with the label UDSM news

UDSM NEWS : YAJAYO YA NAFURAHISHA WAGOMBEA IKS WAAHIDI MAKUBWA, MWENYEKITI WA ZAMANI NAYE ATOA NENO KUELEKEA UCHAGUZI

Image
Na VICTORY  M. Huu ni wakati wakuchagua viongozi mbalimbali katika chuo kikuu cha Dar es salaam  na ndaki mbalimbali   Mambo yamepamba moto huku kila mgombea aki omba kura kwa udi na uvumba pamoja na kuahidi mambo mbalimbali  Katika ndaki ya IKS  Mambo ni moto asikwambie mtu  Katika online exclusive interview,  iliyo fanyika kwa vipindi tofauti baadhi ya Wagombea walileta sera na ahadi zao  Na hapa nimekuwekea kila kitu Mgombea namba  moja alikuwa ni RAMADHANI MZAVA,  MGOMBEA  UKATIBU  IKS Mgombea huyu vipengengele vyake alivyo vipa kipaumbele  1 . Suala la taaluma hasa changamoto za matokeo na changamoto ya mpangilio mbovu wa ratiba  2 . Amezungumzia suala la umoja na mshikamano  3. Kwa mgombea huyu michezo haijaachwa nyuma pia kaipa kipaumbele.              OJWANG HAPPINES   Mgombea viti maalum Iks Mgombea huyu V...

UDSM NEWS :MAFANIKIO YA SERIKALI YA DARUSO 2017/2018 CHINI YA JILILI JOHN JEREMIAH

Image
MAFANIKIO YA SERIKALI YA DARUSO 2017/2018 CHINI YA JILILI JOHN JEREMIAH Awali ya yote ni imani yangu kuwa wana Daruso au wanafunzi wenzangu wa chuo kikuu cha Dar es salaam ni wazima wa afya na mnaendelea vyema katika utekelezaji wa majukumu yenu. Pili nikiwa kama mwana daruso niliepata uhalali kupitia katiba ya daruso ya 2012 ibara ya 9(1) na pia kwa kutimiza matakwa ya katiba hiyo ya daruso ibara ya 9(2). Hivyo kama mwana daruso halali nimeona ni vyema kutumia haki yangu niliyopewa kupitia ibara ya 10(VI) (C) ya kutoa maoni au kueleza fikra zangu na mawazo yangu binafsi dhidi ya Daruso au uongozi wa daruso.Ni fikra hii au tafakuri hii imejikita katika kuchambua utendaji wa viongozi wetu hawa ambao tuliwapa dhamana ili kututumikia ikikumbukwa kuwa uongozi huu unaelekea kwenye ukomo wake hivyo ni vyema kuchambua utekelezaji wao namna walivyowajibika katika uongozi wao hasa kwa kuangazia mihimili yote mitatu ya daruso yaani serikali ya daruso,bunge la daruso(USRC) na mahakama ...

KINGEREZA KINADUMAZA UBUNIFU NA UFANISI KATIKA TAIFA HILI.

Image
Makala Na: Jumaa H Heshima Sitoanza kwa salamu kama ilivyo kawaida ya kile kiitwacho ustaarabu wa Waswahili. Kimsingi hakuna ustaarabu wa Waswahili. Ustaarabu ni wa Waarabu ila tunazo amali tulizozisaliti kwa kuzinasibisha na Uarabu. Basi ya nini kuzibebesha amali zetu adhimu majina yanayozinyima Uafrika wake? Tutafute jina sahihi kuzirejelea amali hizi. Hasira za makala haya ni juu ya athari za "ukoloni lugha'' unavyonyonya na kufifisha ubunifu wa vijana wasomi wa taifa hili pendwa, Tanzania. Sote tunafahamu kuwa Kiswahili ni lugha ya taifa hili, Tanzania. Mwanazuoni mmoja katika kongamano la Kiswahili pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliuliza  swali; ``je, Kiswahili ni lugha ya taifa kikatiba au kimazoea?'' Ukumbi mzima ulitumbua macho pasi na kujibu. Sababu hakuna andiko lolote lile kwenye katiba wala sheria yoyote ile nchini humu inayoeleza na kuelekeza kuwa lugha yetu ya taifa  ni Kiswahili. Hii ni lugha ya taifa kimazoea ni si kimaan...

Taarifa muhimu kwa wanafunzi wa vyuo kutoka Bodi ya Mikopo (HESLB)

Image
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawataarifu wanafunzi wanaonufaika na mikopo kuwa  wanatakiwa kuendelea kuingiza taarifa zao kwa njia ya mtandao kupitia http://olas.heslb.go.tz   hadi tarehe 31 Januari, 2018. Wanafunzi wanufaika wanapaswa kufanya yafuatayo: •    Tembelea mtandao wa http://olas.heslb.go.tz •  Fungua kiunganishi cha “Click here to start” kwenye maelezo ya mwanzo ya kukaribisha. •    Weka namba yako ya mtihani ya Kidato cha Nne na mwaka uliofanya mtihani huo, kwa mfano: S0129.0004.2020 •   Weka namba yako ya akaunti ya Benki kama ilivyowasilishwa HESLB au kama inavyoonekana kwenye “signing sheet” •    Ingiza neno jipya la siri na ulithibitishe. •   Baada ya kuthibitisha, ukurasa wa kuweka picha yako “passport size photo” utafunguka. •    Weka picha yako ya rangi katika ukubwa wa 120×150 •    Wanufaika wapya wa mikopo kwa mwaka wa masomo 201...

KIFUNGO HURU CHA AJIRA

Image
Na: Jumaa H heshima Kifungo kwa maana ya kawaida kabisa ni hali ya kuzuia mtu au kiumbe katika mazingira fulani na kukiwekea mipaka kufika baadhi ya maeneo au kufanya baadhi ya mambo. Neno huru linaashiria hali ya kuamua kufanya jambo mtu alitakalo bila vizuizi. Dhana ya uhuru ni tata kidogo, katika jamii yoyote ile uhuru huwa na mipaka. Mfano kila mtu anao uhuru wa kuvaa nguo aitakayo kwa namna apendavyo ila tu nguo hiyo isioneshe tupu zake. Pia kuna uhuru wa kuongea unalolitaka ila sio kumtukana mtu au kumdhalilisha na kumvua utu wake. Utata uko hapa kwenye kuamua unalolitaka na kisha kuwepo kwa mipaka. Ajira kwa mujibu wa Kamusi ya Karne ya 21 ni kazi ya kulipwa mshara. Maana hii inatuacha na swali juu ya ajira binafsi (self emloyment). Je, muajiriwa analipwa mshahara na nani? Tunaweza kujiridhisha kuwa katika hali hiyo mfanyakazi huyo analipwa mshahara na kazi hiyo anayoifanya na isipomlipa anavyotaka basi ataiacha kama ilivyo kawaida kwa waajiriwa wengine. ...

Wasomi 350 UDSM Wahamia UVCCM

Image
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amepokea jumla ya Wanachma wapya 350 katika Kongamano Maalum lililoandaliwa na Tawi la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Kheri amewataka Vijana wanaopata nafasi za uongozi kuitumia nafasi hiyo kwa ajili ya kuwakomboa wengine na kuacha kutumika na makundi ya watu. “Vijana wengi ambao wameaminiwa wameacha kushughulika na matatizo ya Vijana na yenye tija kwa taifa, wamekuwa wakiendeshwa na watu ambao wanamaslahi yao binafsi” amesema Kheri Amesema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeweza kuwaamini Vijana, hivyo kila kijana wa CCM anabudi kuwaunga mkono viongozi wote Vijana ambao wana nia ya dhati ya kutaka kulifikisha taifa hili pale linapotakiwa liwe. Alimaliza kwa kutoa wito kwa Vijana wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Chaguzi ndogo zinazoendelea na kuifanya CCM ishinde kwa kishindo. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Chama Cha Mapinduzi(UVCCM),Kheri James akizungumza na Wan...

MAISHA YANGU YAPO HATARINI, KUMBUSHO DAWSON, ALIYEIBUA TARIFA ZA NYUFA HOSTEL ZA MAGUFULI

Image
Kumbusho Dawson Ambaye pia ni mbunge wa serikali ya Daruso UDSM , anadai kuanza kufwatiliwa baada ya kuibua taarifa ya nyufa katika magufuli hostel UDSM. KATIKA UKURASA WAKE WAKIJAMII ANAANDIKA #USALAMA_WANGU_UPO_MASHAKANI.  Toka Mwaka jana mwezi wa 12 baada ya mimi kupiga picha katika mojawapo ya  Hostel za  Dr. John Pombe Magufuli iliyokuwa ikionyesha nyufa kumekuwa na watu ambao wamekuwa wakinifuatilia mara kwa mara kila  mahali ninapoenda, (Siwezi kusema kupiga picha za nyufa ndio sababu ya kunifuatilia kwangu au la),  awali nilidhani labda wanashughuli zao tu lakini kilichonishangaza ni kuwa kila siku zinavyoidi kwenda nikikaa sehemu watu hawa nao walikuwa wanakaa umbali kidogo toka nilipo mimi,  nami nikianza kuondoka nikigeuka nyuma nabaini kuwa wananifuatilia.... Siku zinavyozidi kwenda nimebaini watu wale walikuwa na nia mbaya kwangu.  Wiki jana, siku ya Alhamisi nikiwa natoka Mlimani City nilianza kutembea kurudi zangu hoste...

RAISI DARUSO MBIONI KUVULIWA MADARAKA ,SABABU ZATAJWA

Image
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wamemtuhumu Rais wa serikali yao, kwa kukiuka katiba na kutumia nafasi yake kufanya mambo ya hovyo badala ya kutetea maslahi ya wasomi hao ikiwamo kuwasemea waliokosa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka jana. Wasomi hao wamesema Rais huyo John Jeremiah anatumia nafasi yake kuwalazimisha wanafunzi wenzake wakubaliane na mawazo yake binafsi ya kumpongeza John Magufuli kwa kukataa kuongeza muhula wa uongozi kutoka miaka mitano hadi saba. Wamesema masuala hayo anayotaka Rais wa DARUSO hayawasaidia wanafunzi kutatua kero zao ikiwamo baadhi yao kukosa mikopo kwa ajili kugharamia masomo yao. Kutokana na hatua hiyo ya Jeremiah, Bunge la wanafunzi limepanga kuitisha kikao cha dharura ili kukuanya saini za wanafunzi kwa lengo la kumvua madaraka haraka kwa kuwa ameanza kufanya mambo ya hovyo ambayo hayalengi kuwatetea wanafunzi. Makamu wa Rais wa DARUSO, Anastazia Antony na Spika wa Bunge la wanafunzi, Deogratias Mahinyila wamem...