Notes za kiswahili sekondari kidato cha tatu, tungo , uchanganuzi wa sentenzi

TOPIC 2: MJENGO WA TUNGO Maana ya Tungo Tungo ni kipashio cha kisarufi kilichoundwa kwa kuunganisha pamoja vipashio vidogovidogo vilivyo chini yake. Au tungo ni neno au kikundi cha maneno ambacho hudokeza taarifa fulani ambayo huweza kuwa kamili au isiyo kamili. Kwa maana hii, tungo hujengwa na vipashio vidogovidogo kama vile mofimu kuunda neno, neno kuunda kirai, kirai kunda kishazi na kishazi kuunda sentensi. Kama tulivyokwisha kuona hapo juu tungo huanzia neno; rejea aina za tungo. AINA ZA TUNGO Tungo neno : Tungo neno ni tungo ambayo huundwa na vipashio vidogo zaidi ya neno ambayo ni mofimu au fonimu. Mfano; anacheza , kakimbia . Tungo Kirai : ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi lakini ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu. Mfano; mtoto mzuri , kiyama chake , bondeni Tungo kishazi : Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na ku...