Masshele Kiswahili
Wataalamu wa isimuhistoria na isimu linganishi wanatueleza kwamba lugha zote zijulikanazo hii Leo kama lugha za ki Bantu, ikiwemo lugha ya Kiswahili, hapo kale zote zilikuwa na Toni. Baada ya mtawanyiko Mkuu( diaspora) kutokea lugha hizo zikaanza kutofautiana kiasi kwamba hadi hii Leo lugha hizo zimegawanyika katika makundi manne tax McCawley , 1974, na Massamba 2011)

Kwa mujibu wa wataalamu hao kuna lugha ambazo tunaweza kuzihesaby kwamba zina Toni za kiasilia ( purely tonal languages), lugha ambazo zinatoni zilizochombezwa na viinitoni (tone accents languages), lugha ambazo toni zake ni nusu nusu, (tone stress languages) yaani zimo njiani kuachana na matumizi ya toni.); na lugha ambazo zimegeuka na kuwa na mkazo tu ( stress languages)

Lugha ambazo zinatoni asilia huwakilishwa na kisukuma kutoka Tanzania na Toni zake huwa hazitabiriki.

Lugha ambazo Toni zake huchombezwa na viini Toni huwakilishwa na Ci ruuri, kutoka Tanzania na ci toonga kutoka Zambia na Zimbabwe.

Itaendelea
Ongeza mjadala katika sehemu ya comment