Posts

Showing posts with the label Kiswahili

MWANSOKO 1991 MTINDO WA KITAALUMA

Image
Sura ya 2: Mtindo wa kitaaluma Utangulizi Uzoefu wa kusoma makala za kitaaluma na kuhudhuria semina mbalimbali umeonyesha kuwa pamoja na maudhui mazuri ya makala hizi kumekuwa na ukiukaji wa kutosha wa taratibu za kimtindo ambazo zina nafasi muhimu sana katika maandiko na majadiliano yoyote ya kitaaluma. Ingawa mwandishi amekuwa akitoa madokezo ya hapa na pale katika semina hizi kuhusu kanuni za kimtindo na makosa yatokanayo na ukiukaji wa taratibu hizi, hata hivyo suala hili bado linahitaji kuchukuliwa kwa uzito wake kamili hasa kutokana na kuongezeka kwa dhima ya Kiswahili baada ya lugha hii kufanywa lugha ya taifa. Matokeo ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya taifa yamekuwa ni uimarishwaji zaidi wa lugha hii ikiwa ni pamoja na kuipenyeza katika matumizi ya kitaaluma. Masuala ya kitaaluma kwa kawaida hayawi ya nchi moja tu peke yake, bali huhusisha na kushirikisha mataifa mbalimbali. Hii ina maana kwamba tuandikapo makala au vitabu vyetu vya taaluma mbalimbali katika Ki...

UHAKIKI DIWANI YA SHAABAN ROBERT: HASHIKI KITABU HIKI

Kabla ya kuanza kuyachambua masuala mbalimbali yanayojitokeza katika mashairi ya diwani hii ya  Ashiki Kitabu Hiki,  tuichunguze kwanza kwa kifupi historia ya Shaaban Robert. Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari 1909 huko Vibambani, Tanga. Alisoma katika shule mbalimbali Dar es Salaam tangu 1922 hadi 1926, na baada ya hapo alifanya kazi huko Pangani, Longido, na baadaye Tanga. Alifariki tarehe 20 Juni, 1962. Zaidi ya kuandika riwaya na insha, Shaaban Robert aliandika vitabu vingi sana vya mashairi; na kwa kweli ushairi ndio hasa uliompa umaarufu mwandishi huyu. Kati ya vitabu au tuseme diwani za ushairi za mwandishi buyu zipo za  Pambo ta Lugha  (1948), Marudi Mema  (1952),  Uhuru  (1967), Ashiki Kitabu Hiki  (1968),  Mashairi ya Shaaban Rohert  (1968),  Mwafrika Aimba  (1969) na  Sanaa ya Ushairi (1972). Ili kuweza kupata undani wa mashairi ya diwani yoyote ya Shaaban Robert ni vizuri kusoma baadhi kubw...

UTATA WA DHANA YA NENO PDF

Image
DHANA YA NENO DHANA YA NENO NI TATA .  SWALI:    Baadhi ya wanaisimu wanakubaliana kwamba dhana ya neno ni tata. Pinga au kubali                 kauli hii kwa hoja madhubuti. Katika kueleza dhana ya neno ni vyema  tukaanza na kutazama dhana ya mofolojia kwa ufupi. Dhana ya mofolojia imeelezwa na wataalam mbalimbali na miongoni mwao ni: Habwe na Karanja (2012) wanadai kuwa mofolojia ni neno linalotumiwa kumaanisha utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa maneno. Hartman (1972) anaeleza kuwa mofolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulikia uchunguzi na uchambuzi wa maumbo na aina za maneno yaliyo pamoja na historia zake. Hivyo baada ya kuona fasili hizo kulingana na wataalamu mbalimbali, mofolojia yaweza kufasiliwa kama taaluma ya isimu inayojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na ufafanuzi wa maumbo ya maneno. Baada ya kuona fasili mbalimbali za mofolojia kul...

UHAKIKI WA RIWAYA, RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT KUSADIKIKA KUFIKIRIKA NA MAISHA YANGU BAADA YA MIAKA HAMSINI pdf

Image
Riwaya ya kufikirika ni riwaya iliyotungwa na mwandishi mashughuli Shaabani Robert, katika riwaya hii mwandishi anaeleza juu ya mila na desturi zilizopitwa na wakati kuwa hazina nafasi katika kipindi cha sasa. Mwandishi anaeleza kuwa jamii ya watu wakufikirika ilikuwa inaamini juu ya uganga na mambo ya kijadi. Hivyo kupitia mhusika utu busara ambaye alikuwa anaelimu kubwa ya dunia. Utu Busara alijiingiza katika kundi la utabiri ili aweze kuleta mabadiliko katika nchi ya kufikirika. Kutokana na utabiri wake Mfalme na Malkia wanafanikiwa kupata mtoto na baadae Utu Busara tena anakuwa mwalimu wa mtoto wa mfalme na kuanza kumfundisha elimu ya dunia ambayo ni kinyume na matakwa ya mfalme, baada ya kufukuzwa na mfalme, Utu Busara anaamua kujiingiza katika kilimo ambapo ikapelekea kukamatwa kwa kudhaniwa kuwa ni mjinga. Kutokana na elimu na weledi alionao utu busara anafanikiwa kujiokoa kutoka gerezani na kufanikiwa kumponya mtoto wa mfalme kwa kutoa ushauri kuwa apelekwe hospit...