Posts

Showing posts with the label USASA

(WARTS) MARADHI YA NGOZI YANAYOENEZWA KWA NJIA YA NGONO

Image
Baadhi ya maswali tuliyopokea, mengi yalihusu maradhi ya sunzua ambayo kitaalmu yanajulikana kama warts. Sunzua ni ugonjwa wa ngozi unaofahamika na wengi. Ugonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo kitaalamu huitwa human papilloma virus . Karibu asilimia 10 ya wanadamu wamewahi kupata athari za virusi vya ugonjwa huu, achilia mbali kuumwa sunzua. Kwa sababu hiyo ndiyo kusema kila mtu anapaswa kufahamu ugonjwa huu kwa undani ili unapojitokeza awahi hospitali ili kuudhibiti. Virusi vinavyosababisha ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya ngono.Ugonjwa huu hutokea sehemu mbalimbali za mwili, lakini huwatokea wengi sehemu za siri. Sunzua  kama ugonjwa wa zinaa, huathiri sehemu za siri pamoja na njia ya haja kubwa. Wagonjwa ambao wanaishi na Virusi vya Ukimwi wako kwenye mazingira hatarishi zaidi ya kupata  sunzua .  Virusi vinavyosababisha maradhi ya  sunzua  huambukizwa kwa njia ya ngono na ni mara chache huweza kusamba...

USASA USASAMBU SEHEMU YA TANO

Image
  Na WILLIAM HIMU Kwa Mukhtasari Utandawazi una faida nyingi katika maendeleo ya binadamu kijamii, kisiasa na pia kiuchumi ila kwa nchi nyingi za ulimwengu wa tatu utandawazi umekuwa ni kaa la moto.     Sehemu ya Tano B Daktari Twalib: Wasichana wengi hufikia hatua hata ya kujiua pindi wanapokosa msaada kama huu lakini angalia makosa uliyoyafanya na unayotaka kufanya yapi ni makubwa zaidi? Sakina: Ni kweli daktari, hilo tunalielewa vyema lakini huyu ni mwanafunzi anahitaji kusoma. Daktari Twalib:Hapa leo unatoa mimba unajiona ni shujaa, lakini umeshafikiria kama ungepata Ukimwi ungeenda kuutoa vipi? Wewe unavyohangaika kutoa mimba kuna wanawake wenzako ndani ya ndoa wanahangaika kwa waganga usiku na mchana kutafuta watoto… nakushauri usifanye hivyo. Sakina:Daktari nashukuru umetushauri vizuri... Daktari Twalib: Hamtambui tu, kutibiwa sio mpaka mpewe sindano na hata huu ushauri ninaowapa unaponya kuliko dawa. Sakina:Ni kweli daktari… Daktari Twalib:Hiv...

SASA USASAMBU SEHEMU YA PILI

Image
Na WILLIAM HIMU Kwa Mukhtasari Maudhui ya Usasa Usasambu yanagusia maeneo ambayo vijana wengi wanataka kujikita kama sehemu ya burudani Soma ili ufahamu mengi kuhusu vijana hasa wa kike wanavyoathirika na utandawazi SEHEMU YA PILI (Kadri gari lilivyozidi kwenda ndivyo abiria walivyozidi kushuka na kupungua. Mwisho wakabaki Mwanakombo, Mwanaharusi na Mwanawima.) Dereva: Mnaelekea wapi wasomi? (Anauliza huku akiwa anaangalia kwa kutumia kioo kilichopo mbele kabisa juu ya kiti chake.) Mwanakombo:Stonetown (Anajibu kwa mkato.) Konda: Hee! Mnakaa Stonetown mnasoma Chukwani? Si mnapata usumbufu sana! Mwanawima: Ndio maisha yetu haya, huu mwaka wa tatu tunakimbizana na daladala. Mwanakombo:  Matusi na kejeli za madereva na makondakta imekuwa sehemu ya maisha yetu, ndio maana hatuwashangai kwa maneno yenu ya  shombo na roho nyeusi kama zimekolezwa oili chafu. (Anaongea huku amebana pua) eti wa kusoma wametosha. (Anacheka kwa kejeli.) Dereva: O...

SEHEMU YA TATU YA USASA USASAMBU

Image
       Kwa Mukhtasari Kwa kiasi fulani suala la utandawazi limekuwa na matokeo hasi kwa watoto wetu wa kike na kusababisha kuwaathiri kimwili na kiakili. UTANGULIZI SUALA la utandawazi limekuwa ni jambo ambalo hatuwezi kuliepuka katika maisha yetu ya kila siku. Hata hivyo, suala hili limekuwa na matokeo hasi kwa watoto wetu wa kike na kusababisha kuwaathiri kimwili na kiakili. Kuingia kwa utandawazi kumewafanya vijana watumie muda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii na intaneti ambako wanajifunza mambo mengi ya ovyo. Utandawazi una faida nyingi katika maendeleo ya binadamu kijamii, kisiasa na pia kiuchumi ila kwa nchi nyingi za ulimwengu wa tatu utandawazi umekuwa ni kaa la moto kwani kila anayejaribu kulishika lazima limuunguze. Kwa kuona hayo yote mwandishi wa tamthiliya hii ameamua kuifungua macho jamii ili iweze kuchukua hatamu kuwanusuru watoto hasa wa kike. Inaendelea sehemu ya Tatu Mama Mwanaharusi: Kwa nini? Mama Mwanaharusi: (An...