TCRA, MITANDAO YA SIMU, JESHI LA POLISI MPO WAPI? WATANZANIA WANAIBIWA!!

Kutoka kwa moja ya wasomaji wetu Kilio cha haki Na Mwandishi wetu. Ni dhahiri kuwa, mawasiliano kwa njia ya simu yamerahisisha ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi. Katika hatua hii, yapo mambo yanayotumika kinyume na lengo lililokusudiwa ambapo wapo baadhi ya watu wenye kutumia mawasiliano kwa njia za kiuhalifu na kupeana mbinu hasi zenye kujenga chuki, umasikini, hofu na visasi. Kutoka kwa moja ya wasomaji wetu Kwa sasa hapa nchini wapo baadhi ya watu wenye kutumia mawasiliano ya simu kutapeli na kuwahadaa watu kwa lengo la kufanya uhalifu ama kutekeleza dhamira ovu, jambo ambalo linapaswa kukemewa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria. lakini ajabu ni kwamba vyombo vinavyo husika vimeendelea kukaa kimya hadi hali iwe mbaya zaidi Kutoka kwa moja ya wasomaji wetu Simu za mkononi zimekuwa zikitumika sana sio tu kwa ajili ya mawasiliano (kupiga, kupokea ama kutuma ujumbe mfupi wa maneno), bali pia zimekuwa zikitumika kama nyenzo ya kufanyia miamala mbalimba...