MAANA YA UREJESHAJI PDF
TUKI (1990) wanasema urejeshaji ni tendo la kuweka kiwakilishi ambacho huweza kutumiwa kupatanisha kishazi kinachojirejea na kukivumisha kikundi nomino hicho. Yaani kishazi rejeshi kinafanya kazi ya kuvumisha Nomino katika kikundi nomino hicho. Tungo rejeshi ni tungo tegemezi ambayo hutegemezwa kwenye kundi nomino. Wengine wanasema ni uhusianishaji wa maneno kisarufi ambapo tungo rejeshi hurejelea kwenye neno kuu (kisabiki) la kifungu chote. Kuna uhusisano wa moja kwa moja kati ya kile kinachoelezwa katika tungo rejeshi na kile kisabiki kinachorejelewa. Ili kuwa na kishazi bebwa katika sentensi moja inayotokana na sentensi mbili, kishazi kimoja hakina budi kupachikwa ndani ya kishazi kingine yaani kubebwa na kishazi kingine. Hii ni sawa na kusema kuwa kishazi kimoja kinashushwa hadhi na kukipachika ndani ya sentensi nyingine baada ya KN cha sentensi husika. Kishazi rejeshi ni sentensi iliyoshushwa hadhi na kufanya kazi ya KN (ndani ya KN). Mwalimu anaasoma kitabu Kitabu ni kizu...