Kocha msaidizi wa Timu ya Azam Idd Seleman Cheche amesema kuwa wapo tayari kuwavaa 'wajelajela' Tanzania Prisons watakapokutana nao katika mchezo wa ligi utakaofanyika Jumapili ya tarehe 21 Januari, 2018 kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Akizungumza na mtandao wa Azam Fc Cheche amesema kuwa wamerekebisha makosa madogo waliyoyafanya dhidi ya Timu ya Majimaji na kuwa wanatarajia ushindi.
 "Plan yetu Jumapili ni kuhakikisha tunapambana kadri ya uwezo wetu ili kupata matokeo, tumeangalia kitu gani kilitukwanza tukijumuisha na uchovu na tutaangalia jinsi ya kurekebisha ili tusirudie makosa", amesema Cheche.
Cheche amewataja Tanzania Prisons kuwa timu nzuri ambayo watahitaji umakini mkubwa ili kuwashinda.
Timu nzuri
"Tanzania Prisons ni wazuri wanapambana lakini tutatumia udhaifu wao ili tuwaangamize na tuhakikishe tunapata alamu tatu muhimu", ameongeza Cheche.
Mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi mwaka 2018, tayari wapo Jijini Mbeya ambapo wanaendelea na mazoezi kuelekea mchezo huo.
Tanzania Prisons ambao walipata ushindi mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mbeya City wako katika nafasi ya 6 wakiwa na alama 21 nao Azam Fc wakishika nafasi ya pili wakiwa na alama 27 alama mbili nyuma ya vinara Simba SC.