Karibu mpendwa tujifunze maandiko pamoja kwa siku yaleo. Tutajikita katika Kitabu cha nabii Isaya 1:10-17 10 Lisikieni neno la Bwana, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sharia ya Mungu wetu, Enyi watu wa Gomora 11 huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea unafaida gani? Asema bwana. Nimejaa mafuta yawanyama walionona, nami sifurahii damu ya ng'ombe wala ya mwana-kondoo wala ya mbuzi waume 12 mjapo ili kuonekana mbele zangu, ninani aliyetaka neno hili mikononi mwenu, kuzikanyaga nyua zangu? 13 msilete matoleo ya ubatili, uvumba ni chukizo kwangu, mwezi mpya na sabato, kuitaka makutano, siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada. 10: 15-17 15 Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone, Sam, hata muombapo maombi mengi sitasikia, mikono yenu imejaa damu 16 jiosheni, jitakaseni, ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu, acheni kuenda mabaya 17 jifinzeni kutenda mema, takeni hukumu ya haki, wasaidieni walioonewa, m...