Karibu mpendwa tujifunze maandiko pamoja kwa siku yaleo. Tutajikita katika Kitabu cha nabii Isaya 1:10-17

10 Lisikieni neno la Bwana, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sharia ya Mungu wetu, Enyi watu wa Gomora  11 huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea unafaida gani? Asema bwana. Nimejaa mafuta yawanyama walionona, nami sifurahii damu ya ng'ombe wala ya mwana-kondoo wala ya mbuzi waume 12 mjapo ili kuonekana mbele zangu, ninani aliyetaka neno hili mikononi mwenu,  kuzikanyaga nyua zangu? 13 msilete matoleo ya ubatili, uvumba ni chukizo kwangu, mwezi mpya na sabato, kuitaka makutano, siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.

10: 15-17

15 Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha  macho yangu nisiwaone,  Sam, hata muombapo maombi mengi sitasikia, mikono yenu imejaa damu 16 jiosheni, jitakaseni, ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu, acheni kuenda mabaya 17 jifinzeni kutenda mema, takeni hukumu ya haki, wasaidieni walioonewa, mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.

Ndugu, kupitia kwa nabii Isaya Mwana wa Amozi , mwenyezi Mungu wetu anasema na sisi wenye dhambi wazi wazi na kutuambia kwa hakuna hapendezwi na sadaka tuzitoazo hats ikiwa twatoa sadaka kubwa hatutaiona Baraka yake kwakua amesema yeye hashughuliki na sadaka ya mtu mwovu! Mungu sio kama mwanadamu ambaye anaweza kupekea rushwa! La hasha! Mungu wetu hapendezwi na sadaka au matoleo ya mwenye dhambi, hivyo ndugu iwapo tungali katika dhambi na hatujatubu na kuomba msamaha kwa Mungu hatuna kibali cha kumtolea Mungu sadaka na kufanya hivyo ni saw a na kujichosha kwa maana kupitia neno hili anasema "huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea unafaida gani? Kumbuka sodoma na gomora walikuwa katika dhambi nzito na katika maovu hayo hayo walikuwa wakiendelea kumtolea Mungu sadaka na ndipo kupitia Isaya Mungu anawaonya wao pamoja na wote wenye dhambi.

Aidha kupitia neno hili hili Mwenyezi Mungu anena na kusema  kuwa hatayasikai maombi ya mtu maovu! Na hivi ndivyo ilivyo! Kabla ya kufanya maombi kwa Muumba wako yafaa kwanza ujitakase, ndipo update kibali cha kusikilizwa! Nafikiri tumekuwa masguhuda ni Mara ngapi ngapi twafanya maombi lakini hatuoni faida ya maombi hayo? Twafaa tujichunguze kwanza maana Mwenyezi Mungu kupitia neno hili anasema kwa hakika ..." Muombapo maombi yenu sitasikia"  kisha anaendelea kusema "jiosheni, jitakaseni ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu  jifunzeni kutenda mema"  Muumba wetu anatusihi kuacha kutenda uovu ili aweze kuyasikia maombi yetu, anatukumbusha kujitakasa na kujiosha kwa Yale maovu tulonayo! Na mwisho anatusihi kujifunza kutenda mema. Kumbuka ndugu dhambi nikama pamba nzito masikioni mwa Mungu! na hivyo humfanya Mungu  asisikie maombi yetu! Hata hivyo ametupa nafasi ya kuondoa pamaba hiyo kwa kujitakasa kwanza. Mungu hana urafiki na mtenda dhambi Bali hufurahi sana pale mtenda dhambi anapoamua kutubu na kujutia kosa lake  na ndipo utapoona katika mstari wa 18 na kuendelea namna anavyowasamehe wanadamu.
Mwisho
Niandikie kupitia
Info.masshele@gmail.com